Chama Cha Mapinduzi Wilaya Ya Njombe Kimefanikiwa Kufanya Uchaguzi Wa Viongozi Wake Wawili Mwenyekiti Wa CCM Wilaya Na Mjumbe Wa Halmashauri Kuu Ya CCM Taifa NEC Kufuatia Kufariki Kwa Waliokuwa Wakishikilia Zafasi Hizo Ambao Ni Marehemu Adam Msigwa Na Lupyana Fute.
Akitangaza Matokeo Msimamizi Mkuu Na Mchumi Kwa Niaba Ya Kamati Ya Siasa Mkoa Wa Njombe Katika Uchaguzi Huo Alimwimike Sahwi Amemtangaza Osca Michael Msigwa Kuwa Mjumbe Halali Wa Halmashauri Kuu Ya CCM Taifa NEC Baada Ya Kuongoza Kwa Kura Mia Saba 11 Kati Ya Kura 1171 Ya Kura Zote Za Wapiga Kura.
Bwana Sahwi Amesema Nafasi Ya Mjumbe Wa Halmashauri Kuu Ya CCM Taifa NEC Waligombea Watu Watatu Akiwemo Justin Nusulupia Ambaye Amepata Kura 337 ,Geoge Benedict Mng'ong'o Amepata Kura 112 Na Oscar Michael Msigwa Ambaye Ameongoza Kwa Kura Mia Saba 11 Kati Ya Kura Elfu 1171 Dhidi Ya Wenzake.
Katika Hatua Nyingine Msimamizi Huyo Bwana Sahwi Amemtangaza Edward Pius Mgaya Kuwa Mwenyekiti Wa CCM Wilaya Ya Njombe Ambaye Ameongoza Kwa Kura Elfu 1112 Kati Ya Kura Zilizotakiwa Kupigwa 1174 Na Kura 29 Zimeharibika Na Kura Halali 1145 Dhidi Ya Mwenzake Bethren Ngimbudzi Ambaye Amepata Kura 33.
Akizungumza Akiwa Mgeni Rasmi Mbunge Wa Viti Maalumu Mkoa Wa Njombe Na Naibu Waziri Wa Maendeleo Ya Jamii,Wanawake ,Jinsia Na Watoto Dkt Pindi Hazara Chana Pamoja Na Kupongeza Kwa Zoezi Hilo Pia Amesisitiza Wananchi Kujitokeza Kuipigia Kura Katiba Inayopendekezwa Ifikapo April 30 Mwaka Huu.
Naibu Katibu Mkuu Wa CCM Tanzania Bara Na Naibu Waziri Wa Fedha Na Mbunge Wa Jimbo La Iramba Magharibi Mwigulu Lameck Nchemba Amesema Mkuu Wa Wilaya Ya Njombe Anatakiwa Kuwa Makini Na Oparesheni Zinazofanywa Na Halmashauri Za Kusafisha Miji Wilayani Njombe Kwani Wafanyabiashara Wadogo Wakiondolewa Katika Maeneo Yao Hawataweza Kupiga Kura Kuelekea Uchaguzi.
Baadhi Ya Wajumbe Wa Chama Cha CCM Katika Maoni Yao Wameomba Viongozi Waliochaguliwa Kushirikiana Na Wanachama Wote Pasipo Kuwagawanya Ambapo Uchaguzi Huo Wamesema Haukuwa Na Kasoro Kwani Wameridhishwa Na Viongozi Waliochaguliwa.
Uchaguzi Huo Uliwashirikisha Wagombea Watano Walioingia Kwenye Kinyang'anyio Hicho Baada Ya Wengine Kujitoa Na Kufariki Dunia Huku Wajumbe Wakitokea Maeneo Mbalimbali Ya Kata Za Wilaya Ya Njombe Umefanyika Januari 31 Katika Ukumbi Wa Hagafiro Mjini Njombe .
No comments:
Post a Comment