| Wananchi na wanafunzi wa shule ya sekondari Idodi Iringa wakishiriki kuzima moto katika bweni la wanafunzi wa kike shuleni hapo amnbalo lilikuwa likiwaka moto leo asubuhi |
MOTO
mkubwa ambao chanzo chake kinatajwa kuwa ni hitirafu ya umeme
umeteketeza bweni la wasichana katika shule ya Sekondari Idodi
wilaya ya Iringa mkoani Iringa .
Tukio hilo limetokea muda wa saa 4 asubuhi leo wakati wanafunzi wakiwa wakiwa madarasani wakiendelea na masomo.
Alisema kuwa chanzo cha moto huo imesababishwa na hitalafu ya umeme na hakuna mwanafunzi yoyote aliyejeruhiwa na moto huo.
Komba alisema kuwa baada ya jeshi la zimamoto kupata taarifa waliondoka mjini Iringa ambapo ni zaidi ya kilometa 20 hadi ilipo shule hiyo ili kwenda kuzima moto huo.
Hata hivyo aliwapongeza wananchi kwa moyo wa ushujaa kujitolea kuzima moto huo na kuwataka kutoa taarifa mapema pindi majanga ya moto yanapojitokeza katika maeneo yanayowazungu.
“Endapo tungepata taarifa mapema nina amini tungeweza kuokoa vitu vingi zaidi na kuwataka wananchi wasitegemee mtendaji au kiongozi apige simu katika kikosi cha kuzima moto kwani kila mtu ana haki ya kupiga simu 111 katika kitengo cha mawasiliano cha jeshi hilo kuweza kutoa taarifa ya majanga, tumetumia muda mdogo kufika eneo la tukio kutokana ubora wa gari hivyo nawashukuru sana wananchi kwa taarifa na kuweza kuonyesha ushirikiano katika uzimaji wa moto huo usilete madhara zaidi “ alisema
Akizungumzia hasara iliyosababishwa ni kiasi gani Komba alisema hadi sasa hawajapata tathmini kamili ya mali zilizoteketea ila baada ya kazi kukamilika itafahamika ni thamani ya vitu vilivyoungua na kuwekwa wazi kwa wanachi.
Mbunge
wa jimbo la Isimani Wiliam Lukuvi ambako maafa hayo yametokea mbali
ya kuwapa pore walimu na wananchi wa Idodi kwa tukio hilo
bado aliwapongeza wananchi kwa umoja wao kwa kufika mapema
kuthibiti moto huo pamoja na kikosi cha Zimamoto kutoka mjini
Iringa.
Tukio hilo kubwa kulikumba jimbo la
Isimani linaloongozwa na mbunge wake Wiliam Lukuvi ambae ni waziri
wa nyumba na ardhi
Akizungumza
kwa niaba ya mbunge Lukuvi katibu wa mbunge huyo Thom Malenga
alisema kuwa wananchi wamefanyajitihada kubwa katika kuthibiti
moto huo na kuwa mbali ya mali za wanafunzi hakuna madhara kwa
binadamu.
Kuhusu
thamani ya mali zilizoteketea kwa moto huo alisema kwa sasa
bado mapema kujua ila uongozi wa shule hiyo pamoja na wazazi na
wananchi wa Idodi wapo katika kikao ili kujua madhara zaidi na
hasara iliyojitokeza.
Japo alisema hasara za awali zinaonyesha ni vitanda vyote zaidi ya 90 pamoja na baadhii ya vifaa vya wanafunzi vimeteketea kwa moto huo na kuwa jumla ya wanafunzi zaidi ya 110 hawana mahali pa kulala.
Alisema kuwa mwaka 2009 baada ya bweni la wasichana kuteketea kwa moto uongozi wa shule hiyo uliamua kuwabadilishia wanafunzi wa kike bweni na hivyo bweni hili lilikarabatiwa na kupewa wavulana.
Japo alisema hasara za awali zinaonyesha ni vitanda vyote zaidi ya 90 pamoja na baadhii ya vifaa vya wanafunzi vimeteketea kwa moto huo na kuwa jumla ya wanafunzi zaidi ya 110 hawana mahali pa kulala.
Alisema kuwa mwaka 2009 baada ya bweni la wasichana kuteketea kwa moto uongozi wa shule hiyo uliamua kuwabadilishia wanafunzi wa kike bweni na hivyo bweni hili lilikarabatiwa na kupewa wavulana.
Agosti
25/ 2009 jumla ya wanafunzi 13 walipoteza maisha baada ya bweni
lao kuteketea kwa moto na baadhi yao kujeruhiwa kwa ajali kama
hiyo ya moto ambayo kwa kipindi hicho moto huo ulisababishwa na
mshumaa.
No comments:
Post a Comment