Na MatukiodaimaBlog ,kilolo
Askari wa FFU wamelazimika kutumia mabomu ya machozi kutuliza vurugu
kubwa zilizoibuka leo Kati ya Polisi na wananchi wa mjini wa Ilula
katika wilaya ya Kilolo mkoani Iringa kufuatia kifo chenye utata cha
mwanamke mmoja
Tukio hilo limetokea majira ya saa 5 asubuhi Leo na kudumu hadi Majira
ya saa 10 jioni huku kituo cha Polisi kikivunjwa ,bunduki kuporwa na
nyingine kuchomwa moto pamoja na magari matatu na Pikipiki Moja ya
polisi.
Wakielezea tukio hilo wakazi wa mji wa Ilula wameueleza mtandao huu wa
www.matukiodaima.co.tz kuwa chanzo ni askari watatu watatu akiwemo mkuu
wa kituo cha Ilula kwenda kufanya msako wa wananchi wanaokunywa pombe
muda wa kazi.
Hivyo kutokana na tukio hilo mwanamke huyo aliyepoteza Maisha
aliyetambulika kwa jina la Mwanne Mtandi aliamua kukimbia kukwepa
kukamatwa na Polisi hao Kabla ya kukutwa nyuma ya jengo la klabu hicho
cha pombe za kienyeji kilichopo mtaa wa Ilala Mjini Ilula akiwa amekufa.
" Polisi hawa kila siku wamekuwa wakifika hapa klabuni na kukamata watu
na siku kwanza walimkamata marehemu na kumtoza faini ya Tsh 20,000 na
siku ya pili walimkamata yeye na mumewe na kuwatoza faini Tsh 40,000 na
leo walikuwa wakija kumkamata tena na hapo ndipo mwanamke huyo aliamua
kutimua mbio Kabla ya kukutwa amekufa" alisema shuhuda wa tukio hilo
Shida Ngwata.
Huku Mkazi mwingine ambae hakutaka jina lake kutajwa hapa alisema kuwa
Polisi hao walilazimika kutumia mabomu na risasi za moto kutokana na
umati mkubwa wa watu waliojitokeza huku Moja Kati ya bomu likiokotwa
ambalo lilikuwa halijalipuliwa.
Alisema kuwa askari watatu watatu ndio ambao walikuwa wakisakamwa na
Raia hao ambao pia wamevunja vioo vya basi la Upendo kufuatia mkuu wa
kituo Ilula kukimbilia ndani ya basi hilo wakati akifukuzwa na Raia hao .
Diwani wa kata ya Nyalumbu Ally kikunga alisema kuwa alipigiwa simu na
wananchi wake kujulishwa juu na vurugu hizo na Baada ya kufika Eneo la
tukio alikuta mwanamke huyo akiwa mahututi ila hakuweza kupata msaada
toka kwa wananchi wengine ila kumkimbiza hospitali .
Diwani huyo alilishauri jeshi la Polisi kuacha kutumia nguvu zaidi Kwani
alisema Eneo hilo la klabu ni Eneo ambalo pia wananchi wanapata
mahitaji mbali mbali na kuwa mwanamke huyo alikuwa akifanya usafi katika
chumba chake cha biashara ya pombe.
Hata hivyo alisema Raia hao wameharibu Mali mbali mbali pamoja na
nyaraka zote na kuwafungulia mahabusu wote waliokuwemo mahabusu huku
Lori Moja lililokamatwa kituoni hapo likilindwa kuharibiwa kuwa halina
kosa.
Vurugu hizo zilisababisha wasafiri wanaotumia barabara ya Kuu ya Mikoa ya Nyanda za juu kusini kukwama kwa zaidi ya masaa 6 .
Kaimu mkuu wa wilaya ya Kilolo Gerald Guninita pamoja na kamati ya
ulinzi na usalama ya wilaya ya kilolo ilifika eneo la tukio na
kuthibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akiahidi kutoa taarifa kamili
ya Mali zilizoharibiwa na chanzo halisi cha tukio hilo Baada ya kukaa
kikao na viongozi wa jeshi na Polisi na wale wa mji wa Ilula
Japo mwandishi wa habari hizi alishuhudia magari mawili ya Polisi na
Pikipiki yakiwa yamechomwa moto ,gari Moja la askari pia lilichomwa moto
na magari mawili Moja la askari na daladala moja na basi la upendo
kuharibiwa vibaya
Francis Godwin-Iringa
No comments:
Post a Comment