Naibu
Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage akijibu moja ya maswali
yaliyoelekezwa kwenye wizara yake katika kipindi cha maswali na majibu
Januari 30,2015 Bungeni mjini Dodoma.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Janet Mbene akijibu swali Bungeni mjini Dodoma.
Naibu
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dkt. Pindi Chana
akijibu maswali kutoka kwa wabunge mjini Dodoma wakati wa kipindi cha
maswali na majibu.
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla akitoa maelezo wakati wa kipindi cha maswali na majibu Bungeni mjini Dodoma.
Naibu
Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Godfrey Zambi akitoa kauli ya
Serikali kuhusu Mkakati wa Serikali wa Kutatua Changamoto za Soko la
Sukari nchini, Bungeni mjini Dodoma.
Mbunge
wa Viti Maalum (Chadema) Susan Lyimo akichangia hoja ya Kamati za Bunge
za Hesabu za Serikali (PAC), Kamati ya Bajeti na Kamati Hesabu za
Serikali za Mitaa(LAAC) Bungeni mjini Dodoma.
Waziri
Mkuu Mstaafu Edward Lowassa (kushoto) akiteta jambo na Mbunge wa
Kuteuliwa na Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia,
Bungeni mjini Dodoma.
Mbunge
wa Viti Maalum (CCM) Ester Bulaya akichangia hoja ya ya Kamati za Bunge
za Hesabu za Serikali (PAC), Kamati ya Bajeti na Kamati Hesabu za
Serikali za Mitaa(LAAC) jana Bungeni mjini Dodoma.
Mbunge
wa Mkanyageni Mohamed Habibu Mnyaa akichangia hoja Bungeni mjini Dodoma
wakati wa kuchangia hoja za Kamati za Bunge za Hesabu za Serikali
(PAC), Kamati ya Bajeti na Kamati Hesabu za Serikali za Mitaa(LAAC).
Baadhi ya wageni waliohudhuria kwenye ukumbi wa Bunge la Jamhuri bungeni mjini Dodoma.
Picha zote na Hussein Makame-MAELEZO, Dodoma
No comments:
Post a Comment