Add caption
MKUU
wa Chuo Kikuu cha Sayansina Teknolojia Mbeya(MUST) Profesa Mark Mwandosya amewatunuku
vyeti wahitimu1068 katika mahafali ya pili ya chuo hicho katika sherehe
zilizofanyika katikaUkumbi wa Chuo kilichopo Iyunga jijini Mbeya.
Mbali
na Mahafali hayo uongoziwa Chuo hicho umeeleza mikakati yake katika kukabiliana
na upungufu wa Walimuwa masomo ya Sayansi katika Shule za Sekondari nchini, kwa
kuanzisha kitengocha Elimu ya sayansi.
Hayo
yalibainishwa na Makamu Mkuu wa Chuo kikuu cha Sayansi naTeknolojia
Mbeya(MUST),Profesa Joseph Msambichaka, katika Risala yake wakati wamahafali ya
Pili ya Chuo hicho, ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Mkuu wa Chuohicho Profesa
Mark Mwandosya(Mb) na Waziri wa nchi Ofisi ya Rais kazi maalum.
Profesa
Msambichaka alisemauongozi wa Chuo unaendelea na mikakati na matayarisho ya
kuanzisha Chuo chaelimu ya sayansi kwa ajili ya kufundisha walimu wa sayansi
watakaofundishashule za Sekondari ili kupunguza changamoto ua upungufu wa
walimu wa Sayansinchini.
Alisema
mkakati huo unawezekanakutoka na Chuo kufanikiwa kuanzisha vyuovitatu
katika kipindi cha Mwaka mmoja ndani ya Kampasi kuu ya Chuo cha Sayansina
Teknolojia Mbeya ambavyo ni Chuo cha Uhandisi na Teknolojia, Taasisi yaSayansi
na Teknolojia na Skuli ya mafunzo ya Biashara.
Aidha
alitoa wito kwa Wahitimukutumia ujuzi walioupata katika kuchangia kuongeza kasi
ya maendeleo ya taifasambamba na kuwa mabalozi wazuri wa Chuo cha Sayansi na
Teknolojia Mbeya katikakuendeleza matumizi ya sayansi na Teknolojia na hivyo
kuleta ufanisi katikashughuli za ujenzi wa taifa.
Kwa
upande wake Mwenyekiti waBaraza la Chuo, Profesa Penina Mlama akimkaribisha
Mkuu wa Chuo cha Sayansi nateknolojia Mbeya, Profesa Mark Mwandosya kuwatunuku
vyeti wahitimu alisemaMahafali hiyo ni ya pili tangu kuanzishwa na kupandishwa
hadhi kutoka Taasisiya Sayansi na Teknolojia hadi kuwa Chuo kikuu. Alisema
jumla ya wahitimu 1068watatunukiwa vyeti ambapo kati yao wahitimu 821 ni wa
ngazi ya Stashahada yakawaida na wahitimu 246 ni wa ngazi ya Shahada ya Kwanza
katika fani zaUhandisi wa Kompyuta, Uhandisi wa mitambo, uhandisi ujenzi,
uhandisi umeme,usanifu majengo na uongozi wa biashara.
Profesa
Mlama aliongeza kuwakatika takwimu za wahitimu mwaka huu zinaonesha kuwa kati
ya wahitimu 1068wahitimu wa kike ni 160 sawa na asilimia 15 ikilinganishwa na
awamu iliyopitaambayo ilikuwa na asilimia 10 ya wahitimu wa kike hivyo kufanya
kuwa naongezeko la udahili wa watoto wa kike kuongezeka kwa asilimia 5.
Alisema
pamoja na ongezeko hilobado inatakiwa jitihada za maksudi ili kuongeza udahili
wa wanafunzi wa kikekatika Chuo hicho ambapo pia aliupongeza Mfuko wa elimu
Tanzania(TEA) kwamchango wao mkubwa wa ruzuku ulivyowawezesha wanafunzi wa kike
zaidi kujiungana Chuo hicho.
Mwisho.
|
No comments:
Post a Comment