NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII,WANAWAKE,JINSIA NA WATOTO PINDI HAZARA CHANA AKIPEANA MKONO NA AFISA ELIMU TAALUMA MKOA WA NJOMBE MINDUVA HASSAN BAADA YA KUKABIDHIWA VITABU.
MBUNGE VITI MAALUMU MKOA WA NJOMBE NA NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA MAENDELEO YA JAMII,WANAWAKE,JINSIA NA WATOTO PINDI HAZARA CHANA AKIKABIDHI MSAADA WA VITABU HIVYO KWA AFISA ELIMU TAALUMA MKOA WA NJOMBE
MBUNGE WA VITI MAALUMU MKOA WA NJOMBE AMBAYE NI NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII,WANAWAKE,JINSIA NA WATOTO DKT PINDI HAZARA CHANA AKIWA OFISINI KWAKE MKOANI NNJOMBE
Mbunge Wa Viti Maalumu Mkoa Wa Njombe Na Naibu Waziri Wa Maendeleo Ya Jamii,Wanawake Jinsia Na Watoto Pindi Hazara Chana Leo Amekabidhi Vitabu Vya Masomo Mbalimbali Vikiwemo VYa Sayansi Vyenye Zaidi Ya Shilingi Milioni Kumi Katika Ofisi Ya Elimu Mkoa Wa Njombe Ili Kutatua Changamoto Zinaikabili Sekta Hiyo.
Akizungumza Na Waandishi Wa Habari Wakati Wa Kukabidhi Vitabu Hivyo Kwa Afisa Elimu Mkoa Wa Njombe Dkt Pindi Hazara Chana Amesema Kuwa Serikali Imekuwa Ikikabiliana Na Jitihada Mbalimbali Za Kutatua Changamoto Za Kukosekana Kwa Vitabu Ambapo Amesema Kuwa Hatua Hiyo Ni Kuonesha Mfano Kwa Wadau Wengine Kuchangia Mahitaji ya Elimu Vikiwemo Vitabu.
Dkt Chana Amesema Kuwa Hatua Hiyo Ya Kukabidhi Vitabu Hivyo Kwa Shule Mbalimbali Za Msingi Na Sekondari Mkoani Njombe Muendelezo Wa Ofisi Ya Mbunge Kuhakikisha Inaonesha Mfano Kwa Wadau Wengine Wa Elimu Kuona Umuhimu Wa Kusaidia Sekta Ya Elimu Ambapo Ametaka Wanafunzi Kusoma Kwa Bidii Na Kuongeza Ufaulu Shuleni Kutokana Na Changamoto Ya Uhaba Wa Vitabu Inakwenda Kutatuliwa.
Aidha Dkt Chana Amewataka Wananchi Kuwapeleka Shule Watoto Wao Kujiunga Na Masomo Ya Shule Za Msingi Na Sekondari Na Kwamba Wizara Ya Maendeleo Ya Jamii Inakemea Tabia Ya Mimba Kwa Wanafunzi Shuleni Ambapo Amesema Vyombo Vyenye Sheria Vinatakiwa Kuchukua Hatua Kali Kwa Watakaobainika Kusababisha Mimba Kwa Watoto Wa Shule.
Akipokea Msaada Huo Wa Vitabu Afisa Elimu Taaluma Mkoa Wa Njombe Minduva Hassani Amemshukuru Mbunge Huyo Kwa Kusaidia Msaada Huo Na Kwamba Sekta Ya Elimu Kwa Wakati Huu Ipo Kwenye Mpango Wa Matokeo Makubwa Sasa BRN Na Kwamba Serikali Inatoa Kiasi Cha Fedha Kwaajili Ya Kununua Vitabu Shuleni Lakini Bado Havitosherezi .
Mwalimu Hassan Amesema Mkoa Wa Njombe Ni Miongoni Mwa Mikoa Inayofanya Vizuri Katika Elimu Ya Msingi Na Sekondari Na Hivyo Wadau Wanatakiwa Kuwa Na Moyo Wa Uzarendo Kusaidia Shule Mbalimbali Ili Kutatua Baadhi Ya Changamoto Zinazoikabili Sekta Ya Elimu Ikiwemo Kusaidia Vitabu,Ujenzi Wa Nyumba Za Walimu Na Kupeleka Samani Za Shule.
Hatua Ya Mbunge Wa Viti Maalumu Mkoa Wa Njombe Dkt Pindi Hazara Chana Kukabidhi Vitabu Vya Masomo Mbalimbali Vikiwemo Vya Masomo Ya Sayansi Kwa Mkoa Wa Njombe Ni Muendelezo Wa Jitihada Za Mbunge Huyo Kusaidia Sekta Ya Elimu Ambapo Siku Chache Zimepita Amekabidhi Bati Hamsini Kwa Shule Za Sekondari Mkoani Hapa.
No comments:
Post a Comment