Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Sunday, September 28, 2014

 HAPA NI NJE YA UWANJA WA KANISA LA KIINJILI LA KILUTHEL TANZANIA MELINZA  KWENYE MITI KANDO YA BARABARA KUU YA NJOMBE SONGEA
 HAWA NI WANANCHI WA MTAA WA MELINZE WAKISHUHUDIA TUKIO LA KUFARIKI KWA MAREHEMU HUYO BWANA Evaristo Mgeni




 MKAZI WA MTAA WA MELINZE AKIWA ENEO ALILOLALA USIKU WOTE HADI ALIPOKUJA KUTAMBULIWA NA WANANCHI




 ASKALI  POLISI WAKIUCHUKUWA MWILI WA MAREHEMU TAYARI KWA KUUPELEKA HOSPITALI YA KIBENA



Na Michael Ngilangwa -Njombe

Mtu Mmoja mkazi wa mtaa wa Melinze Evarist Mgeni amekutwa akiwa amefariki dunia

katika uzio wa mlango wa Kuingia kanisa la Kiinjili la Kiluthel Tanzainia Usharika wa

Melinze  mapema  leo Huku chanzo cha Tukio hilo kikishindwa kufahamika mara moja.

Wakizungumza na Uplands fm Baadhi ya mashuhuda wa Tukio hilo wamesema wameweza

kumuona marehemu  Evarist Akiwa amelazwa kifudifudi kwenye miti ya Hekya ya kanisa

la Kiinjili la Kiluthel Tanzania la Melinze Ambapo wamepeleka taarifa kwa viongozi wa

mtaa ndipo nao wakapeleka taarifa hizo kwa jeshi la polisi na kuimarisha usalama.

Wamesema kuwa tukio hilo huenda likahusishwa na mauaji Nakwamba taarifa  kamilii

kama ameuwawa ama amefariki mwenyewe zitathibitishwa na Mganga Mkuu wa Hospitali

ya Kibena ambako Mwili wa Marehemu huyo umepelekwa kwa uchunguzi zaidi Ambapo

wameomba serikali za mitaa ziendelee kuimarisha ulinzi shirikishi ili kutokomeza matukio

kama hayo.

Akizungumza akiwa eneo la Tukio Afisa Mtendaji wa Kata ya Mjimwema bwana Gehazi

Mkongwa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba chanzo cha Tukio hilo bado

kinaendelea kuchunguzwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe Ambapo tukio limetokea

majira ya saa isiyofahamika ya  usiku wa kuamukia leo.

Aidha bwana Mkongwa amewaomba wananchi kuonesha ushirikiano kwa viongozi wao

katika kutoa taarifa za matukio yanapokuwa yamejitokeza katika maeneo yao Kwani

kumekuwa na baadhi ya wananchi hushindwa kutoa taarifa kwa wakati kwa viongozi

matukio ya mauaji yanapokuwa yametokea.

Matukio ya Mauaji yamekuwa yakijitokeza kwa baadhi ya maeneo katika halmashauri za

Mkoa wa Njombe Huku wengine wakivamiwa,kujeruhiwa na kupolwa mali zao Ambapo

Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe limekuwa likihamasisha viongozi kwa kushirikiana na

viongozi wa mitaa kuunda ulinzi shirikishi lili kuzuaiya matukio kama hayo.

No comments:

Post a Comment