Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Thursday, September 25, 2014

MBUNGE MSTAAFU WA MUFINDI KASKAZINI JOSEPH MUNGAI AMEAHIDI KUCHANGIA MILIONI 20,MKUU WILAYA MUFINDI EVARISTA KALALU NAYE ATOA AHADI YA BATI 20 KWAAJILI YA KUKAMILISHA UJENZI WA KANISA LA KKKT MALANGALI













 ASKOFU WA KANISA LA KIINJILI LA KILUTHEL TANZANIA DAYOSISI YA KUSINI JAPHET MENGELE AKIZUNGUMZA  AKIWA KATIKA KANISA ALILOANZA KULIJENGA MAREHEMU THOMASI BANGU MALANGALI






 WANANCHI MBALIMBALI WAKIWA MAKINI KUSIKILIZA NENO LA MUNGU AMBALO LINATOLEWA NA MAASKOFU KATIKA KANISA HILO SIKU YA MSIBA WA MZEE BANGU





 VIJANA MBALIMBALI AKIWEMO WILIARD MAIM,AGREY NYASI WAKIWA NA WENZAO KWENYE MSIBA HUO

 NDUGU WA MAREHEMU AKIWEMO MKE WA MAREHEMU BANGU NA WATOTO WAKE

 HILI NDILO KANISA AMBALO MAREHEMU ALIANZA KULIJENGA NA HAPA LIPO HATUA ZA MWISHO


 HAPA SAFARI YA KUELEKEA MAKABURINI  KUMZIKA MZEE BANGU

Mbunge Mstaafu Wa Mufindi Kaskazini Joseph Mungai Ameahadi Kuchangia Milioni 20 Huku Mkuu Wa Wilaya Ya Mufindi Mkoani Iringa Bi.Evarista Kalalu Akiahidi Kupeleka Bati 20 Kwaajili Ya Kukamilisha Ujenzi Wa Kanisa Ambalo Alianzisha Kulijenga Marehemu Mwalimu Mstaafu Tomasi Asangye Bangu Malangali.

Akizungumza Mbele Ya Maaskofu Mbalimbali Tanzania Wakiongozwa Na Askofu Wa Dayosisi Ya Kusini Japhet Mengele Ambao Wamefika  Kuuzika Mwili Wa Marehemu Thomas Bangu, Mbunge Mstaafu Joseph Mungai Amesema  Kwa Kutambua Jitihada Za Marehemu Huyo Za Kufundisha Na Kuendeleza Elimu Ya Ufundi Stadi Wakristo Na Wananchi Kata Ya Malangali Wanatakiwa Kuiga Mfano Wake.

Aidha Bwana Mungai Amesema Kuwa Marehemu Bangu Alianza Kujenga Kanisa La  Kiinjili La Kiluthel Tanzania Katika kijiji cha Mwilavila Kata Ya Malangali   Ili Kusaidia Kupunguza  Umbari Mrefu Kwa Wakristo Wa Kata Hiyo Ambao Wamekuwa Wakisafiri Hadi Kijiji Jirani Cha Isimikinyi Kupata Huduma Za Kiroho.

Mkuu Wa Wilaya Ya Mufindi Mkoani Iringa Evarista Kalalu Amesema  Serikali Inatambua Uwepo Wa Marehemu Mwalimu Mstaafu Thomas Bangu Ambapo Amesema Wananchi Na Wadau Mbalimbali Wa Huduma Za Kiroho Wanatakiwa Kuunga Mkono Jitihada Hizo Pamoja Na Wanafunzi Kuthamini Masomo Ya Ufundi Stadi Kwa Manufaa Yao.

Awali Akiwakaribisha Wageni Mbalimbali Katika Kanisa Ambalo Marehemu Mwalimu Thomas Bangu Alianza Kujenga  Askofu Wa Kanisa La kiinjili la  Kiluthel Tanzania Dayosisi Ya Kusini Japhet Mengele Akiwa Na Mkuu Wa Kanisa La Kiinjili La Kiluthel Tanzania Askofu Dkt Alex Malasusa Wamesema  Wakristo Na Wadau Wa Dini Wanatakiwa Kuchangia Michango Mbalimbali Ili Kukamilisha Ujenzi Wa Kanisa Hilo Ambalo Lipo Katika Hatua Za Mwisho Kukamilika.

Samwel Thomas Bangu Na Washiriki Mbalimbali Akiwemo Mwalimu Judith Kisinini Wakatoa Historia Ya Marehemu Thomas Bagu Kwamba Alizaliwa June 29 Mwaka 1918 Akiwa Katika Kijiji Cha Mdandu Wilaya Ya Wanging'ombe mkoani Njombe Ambapo Alikuwa Mwalimu Wa Ufundi Stadi Katika Shule Ya Sekondari Malangali  Wilayani Mufindi Mkoani Iringa Hadi Alipo Staafu Mwaka 1973.

Marehemu Thomas Asangye Bangu alifariki mnamo sept 20  na kuzikwa septemba 24,2014  katika makaburi yaliyopo kijiji cha Mwilavila kata ya Malangali Wilayani Mufindi na Kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali Nchini Tanzania  wa serikali,Siasa na Kidini.

No comments:

Post a Comment