MAMLAKA
ya mafunzo ya ufundi stadi Nchini (VETA) Nyanda za Juu kusini,
Imefunga vyuo saba vilivyopo katika mkoa wa Njombe na Iringa kwa kosa la
kutokidhi vigezo ukiwemo usajili wa vyuo hivyo.
Ni kufuatia kufanya ziara ya kushitukiza iliyofanywa na Veta. Akiongea na baadhi ya wamiliki na wanafunzi wa vyuo mratibu wa Veta nyanda za juu kusini Bw. john Mwanja amesema kuwa kutokana na wimbi la kuanzishwa kwa vyuo ni vema wazazi wakaanza kufuatilia usajili wa chuo ili kuepusha hasara ya muda pamoja na fedha pamoja na vyeti wanavyopata havitambuliwi na serikali hivyo inawawia vigumu kupata ajira.
Prosper Mfugale ni Mwandishi wa Habari wa kituo cha Ebony Fm & Clouds Fm akiendelea kufuatilia kwa ukaribu tukio hilo.
Majengo ya chuo cha Mosemi tawi la Njombe. Jengo la chuo cha Musoma Utalii kilichopo eneo la Mgendela Mjini Njombe. Moja ya darasa lililopo katika chuo hicho. Bw. john Mwanja akiwambia ukweli baadhi ya wanafunzi kuwa wamekuwa wakiibiwa fedha zao na kuwataka kuwaambia na wenzao wenye lengo la kujiunga na chuo.
Hakuna aliyekuwa na Furaha mara baada kupokea kwa taarifa hiyo. Abrubakal Suleiman alisema kuwa yeye ni mkazi wa mjini Iringa alienda Mkoani Njombe Mara baada ya kuona tangazo ambalo halisadifu hali halisi iliyopo chuoni hapo.

Hili ni jiko lililopo katika moja ya chuo ambacho inasemekana ilikuwa nyumba ya mtu
Mratibu wa vyuo hivyo akiendelea na ukaguzi katika chuo cha Eckross kilichopo sabasaba Mjini Njombe.
Akivitaja vyuo hivyo Vilivyofungiwa Mratibu huyo amesema kuwa ni
Capricon Collage,Iringa Hotel and Tourism Collage vya Mjini Iringa, Chuo
cha Mufindi
Tourism Collage cha Mufindi, na Njombe ni Mosemi Collage, Musoma Utalii,
Hokaido VTC na Eckross Collage.
Katika
hatua Nyingine aliwataka wazazi makini wanawapeleka watoto wao chuo cha
kati kuwa kuangalia usajili wa vyuo hivyo na kuzitaja sifa ambazo za
chuo kilichosajiliwa amesema kuwa ni pamoja na Majengo na vifaa
vitakavyowasaidia wanafunzi kufanya kazi jambo ambalo limekuwa ni tatizo
kwa vyuo vingi vilivyokosa sifa ya usajili.
No comments:
Post a Comment