Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Friday, August 22, 2014

MBEYA YETU LEO IMEMULIKA BARABARA KOROFI AMBAYO VIONGOZI WA NGAZI ZA JUU NA WATUMISHI WA SERIKALI HUITUMIA KWA KIASI KIKUBWA.


Hiki ni kipande kifupi sana cha barabara ambacho hakina hata Robo Kilometa , kipande hiki cha barabara ni Muhimu sana kwa sababu Magari ya Mahakama Kuu yanapita hapa, Mahabusu wanapopelekwa Mahakamani wanapitishwa hapa, RPC anapita hapa, Majaji wanapita hapa, Wanasheria wa Serikali wanapita hapa, Benki kuu wanapita hapa, wanafunzi na wananchi wanapita hapa. Lakini cha kushangaza na kustaabisha zaidi kakipande haka ka Barabara kamesahaulika kabisa hakuna anayekitazama ni miaka kadhaa imepita hakuna ukarabati wowote.
Kwa wahusika wa Miundo Mbinu ya Barabara Jiji la Mbeya hivi Kero hii mnaiona
Hiki ni kilima ambapo Mbele jengo kubwa la Ghorofa ni Mahakama Kuu kanda ya nyanda za juu kusini , hapo hapo ndipo unaelekea Benki kuu na Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Lakini Barabara ndio kama inavyo onekana.
 Hili ni Moja ya Korongo kubwa ambalo lipo katika kipande hicho cha barabara 
 Hapa pana Afadhali kidogo
 Haka kasehemu kamechimbika 
 Hapa hakuna hata pakukwepea
 Hakuna unafuu eneo hili
 Makorongo mwanzo mwisho
 Magari yanapishana kwa Shida.

USHAURI KUTOKA MBEYA YETU, WAKATI JIJI WANAENDELEA KUJIPANGA KATIKA HILI BASI CHUO CHA MAFUNZO  MAGEREZA KAMA KUNA WAKANDARASI WASAIDIE BASI HATA KUWEKA KIFUSI HAPO.

Picha zote na Mbeya yetu

No comments:

Post a Comment