Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Monday, August 18, 2014

KINONDONI YATWAA UBINGWA ARS 2014




 Naibu katibu mkuu wa wizara ya habari ,utamaduni na michezo Profesa Elisante Ole
Gabriel akimkabidhi kombe la ubingwa wa Airtel Rising Stars 2014 nahodha wa
timu ya wasichana ya Temeke Fatuma Issa baada ya kuibuka mabingwa. naeshudia ni
Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania Sunil Colaso.




 Makamu mwnyekiti wa chama cha soka cha wanawake Tanzania Rose Kisiwa akimkabidhi kombe la ubingwa wa Airtel Rising Stars 2014 nahodha wa timu ya mkoa wa kisoka
Kinondoni Fred Mazuri  Baada ya kuibamiza
Ilala 5 – 3, Jumapili jijini Dar-es-Salaam.





Wachezaji  wa timu ya mkoa wa kisoka ya Kinondoni wakishangilia ubingwa wa Airtel Rising
Stars 2014 baada ya kuifunga timu ya Ilala 5 – 3, Jumapili jijini
Dar-es-Salaam.


Kinondoni yatwaa ubingwa ARS 2014

Timu ya Kinondoni wavulana imetwaa uchampioni wa
mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars kwa
kuifunga timu ngumu ya Ilala 4-2 kwa changamoto ya mikwaju ya penati baada ya
sare ya 1-1 katika muda wa kawaida wa dakika 90.


Mechi hiyo iliyotanguliwa na shamra shamra za
maandamano na halaiki, ilikuwa yenye upinzani mkali na baada ya kosa kosa za
hapo na pale Kinondoni walipata goli katika dakika ya 31 kupitia kwa Kassim
Kitwana kwa shuti kali la mbali lililomshinda mlinda mlango wa Ilala Sulum
Siasa.


Goli hili lilibadili kasi ya mchezo huku Ilala
wakitafuta goli la kusawazisha na juhudi zao zilifanikiwa kuzaa matunda katika
dakika ya 40 baada ya kutoke piga ni kupege golini mwa timu ya Kinondoni na
mchezaji hatari Juma Yusufu kufunga kwa huti la karibu.


Kipindi cha pili kilianza kwa kushambuliamba kwa zamu lakini hakuna timu iliyofanikiwa kupata goli la kuongoza hadi dakika ya mwisho. 

Ndipo refa akaamua kumaliza ubishi kwa penati.Katika penati tano, Kinondoni walifunga kupitia kwa Abdul Malangali, Milaji Gwangaya, Omri Rashid na Abubakari Nuru wakati Kassim Kitwana alipaisha. Kwa upande wa Ilala waliofanikiwa kufunga ni Abdul Bitebo na Rashid  Mohamed wakati Maisala Adam na nahodha wa timu Shaban Zuberi walikosa.

Akifunga fainali hizo za taifa za Airtel Rising
Stars, mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo Professor Elisante Ole Gabriel kwa niaba ya Naibu Waziri wa wizara hiyo
Mheshimiwa Juma Nkamia, aliipengeza kampuni ya Airtel kwa kujitokeza kusaidia
maendeleo ya soka hapa nchini.


Alitoa wito kwa vijana kuzingatia nidhamu katika michezo na kujituma ili kupata mafanikio na kusema kuwa katika dunia ya leo soka ni chanzo cha ajira kwa vijana wengi. Pia alisema kuwa kufanikiwa kwao kutaiwezesha Tanzania kufahamika zaidi kimataifa. Naye Mkurungenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania Sunil Colaso amesisitiza nia thabiti ya kampuni yake kuendelea kudhamini mashindano ya vijana ya Airtel Risig Stars.

No comments:

Post a Comment