MGENI RASMI ERNEST MKONGO KWA NIABA YA MKUU WA MKOA WA NJOMBE KEPTAIN MSTAAFU ASERI MSANGI
WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI MAPOGORO WILAYANI LUDEWA
BURUDANI YA VIKUNDI MBALIMBALI VYA NGOMA NA KWAYA VIKITUMBUIZA
BEPPE BUSCEGHE ACRA PROJECT MENEJA AKITOA HOTUBA YAKE YA UTEKELEZAJI WA MRADI HUO KABLA YA KUKABIDHI
WANANCHI WA KATA TATU ZA LUDEWA MLANGALI,MAWENGI NA MILO
KATIBU WA JUMUIYA YA UMEME-LUMAMA PHILBERT L.KAYOMBO AKITOA NASAHA KIDOGO BAADA YA KUKABIDHIWA
MWENYEKITI WA KIJIJI CHA MAPOGORO BWANA HERMAN LUBEN MCHIRO AKIFUNGUA MKUTANO
KAIMU MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA LUDEWA HORACE W. KORIMBA AKIZUNGUMZA NA WANANCHI JUU YA KUUTUNZA MRADI HUO USISIMAME NA KUHARIBIWA MIUNDOMBINU YAKE
MENEJA KAMPUNI YA TANWAT KIMASA SHEJA AKIIWAKILISHA KAMPUNI YA TANWAT INAYOHUSIKA NA UPANDAJI MITI NA UTUNZAJI MAZINGIRA
KATIBU TAWALA WILAYA YA LUDEWA STEPHAN A.ULAYA
KIKUNDI CHA NGOMA YA MTULI MAPOGORO NA MAWENGI
HAWA NI WANANCHI WA KATA TATU ZINAZONUFAIKA NA MRADI HUO WA UMEME LUMAMA
MENEJA CRDB MKOA WA NJOMBE WA KATIKATI AKIWA NA WENZAKE WAKATI WA KUKABIDHI MRADI HUO
DIWANI WA KATA YA MILO BWANA DAUD THOMAS MWAFYUMAH
ACRA PROJECT MENEJA BWANA BEPPE BUSCEGHE KUTOKA NCHINI ITALI
WITGAL NKONDOLA AFISA WA MAJI BONDE LA ZIWA NYASA LA TUKUYU-MBEYA
MENEJA CRDB MKOA WA NJOMBE
FURAHA KUBWA KWA WANANCHI KWA KUPATA MRADI HUO
Shirika lisilo la kiserikali la ACRA Mkoa wa Njombe jana limekabidhi mradi wa umeme kwa Bodi ya Jumuiya ya mradi wa umeme Lumama Wenye thamani ya shilingi bilioni sita unaozalisha kilowati mia tatu za umeme.
Mradi huo wa umeme ulioanza kutekelezwa na shilika hilo la ACRA tangu mwaka 2006 unahudumia vijiji nane vya kata tatu za Mlangali,Milo na Mawengi Wilayani Ludewa tayari umeanza kuwanufaisha wananchi wa kata hizo Ambao wamekwisha kuingiziwa kwenye nyumba zao,Viwanda na zahanati.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Njombe Keptain Mstaafu Aseri Msangi baada ya kupokea mradi huo,Kaimu Mkuu wa mkoa wa Njombe Ernest Mkongo amewataka wananchi kutunza vyanzo vya maji na mazingira ili kutililisha maji kwa wingi na kuongeza kilowati za umeme kutoka kilowati mia tatu na kufikia kiwango cha mega wati na wananchi wa vijiji vingine wanufaike.
Aidha bwana Mkongo amewataka wananchi kwa kushirikiana na viongozi wa vijiji,kata na Jumuiya ya mradi huo wa umeme Lumama kuhakikisha wanatoa taarifa sehemu husika juu ya wanaosababisha uharibifu wa mazingira na vyanzo vya maji kwa kuchoma moto na kulima kwenye vyanzo hivyo ili maji yasipungue kwenye vyanzo vyake.
Awali akikabidhi mradi wa umeme Lumama Meneja wa mradi huo kutoka Shirika la Acra bwana Beppe Busceghe amewataka wananchi wa kata hizo tatu za Mlangali,Milo na Mawengi Wilayani Ludewa kutunza miundombinu ya umeme na vyanzo vya maji ili udumu kwa muda mrefu.
Bwana Busceghe amesema kwa kipindi ambacho mradi huo umekuwa katika hatua za utekelezaji, mwaka 2006 mto Kasongo ambao unazalisha umeme huo ulikuwa nauwezo wa kutiririsha lita mia sita kwa sekunde Ambapo kwa sasa kiwango kimepungua na kufikia lita mia tatu kwa sekunde.
Amesema pia wamefanikiwa kutekeleza miradi mingine ikiwemo elimu kwa kujenga na kukarabati madarasa katika shule za msingi,kuchimba visima,ujenzi wa vyoo,kuingiza umeme kwenye taasisi za serikali ikiwemo zahanati,mafunzo kwa baadhi ya walimu,kujenga majiko ya kisasa kwaajili ya shule za msingi,pamoja na kugawa vitabu na mahitaji mengine wameweza kuyafanya.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Ludewa bwana Horacy Kolimba ameahidi kusimamia utunzaji wa mazingira na vyanzo vya maji na kuwataka wenyeviti,watendaji na madiwani wa kata kuhakikisha wanasimamia na kuchukua hatua kwa atakaye kiuka agizo la serikali.
Katibu wa jumuiya ya mradi wa umeme Lumama bwana Philibet Kayombo amesema jumuiya hiyo itahakikisha mradi huo hausimami na kusema kuwa shirika la ACRA pamoja na kutekeleza mradi wa umeme lakini wamesaidia kuwapeleka walimu chuo cha klelu kwaajili ya mafunzo na kutoa mahitaji mbalimbali ikiwemo kompyuta arobaini katika shule za sekondari na kutekeleza miradi ya maji.
Mradi wa umeme Lumama unazalishwa kwenye chanzo cha Mto Kasongo Wilayani Ludewa ambapo nao wananchi wakatoa maoni yao kuhusu mradi huo kwa kutaka jumuiya ya umeme lumama kupeleka ankra za umeme karibu nao ili kupunguza kusafiri umbali mrefu kuliko kwenda kulipia kata ya mawengi ambako ni gharama zaidi.
No comments:
Post a Comment