HILI NI GARI LA DIWANI WA VITI MAALUMU ANJELA MWANGENI AMBALO LIPO KUSHUSHA MAHINDI NA MAHITAJI MENGINE KAMA SUKARI,MAHINDI NA MAHARAGE
DIWANI MWANGENI AKISAINI KITABU CHA WAGENI OFISINI KWA MWALIMU MKUU MARA BAADA YA KUWASILI SHULENI HAPO
AFISA TARAFA YA NJOMBE MJINI AKIWA OFISINI KWA MWALIMU MKUU AMBAE ALIONGOZANA NA DIWANI HUYO
DIWANI VITI MAALUMU ANJELA MWANGENI AKIWA TAAYRI KASAINI KITABU CHA WAGENI TAYARI KWA KUKABIDHI MSAADA HUO
KATIBU WA VIJANA WA CCM WILAYA YA NJOMBE HIMID TWEVE NAE ALIONGOZANA NA DIWANI HUYO
AFISA TARAFA WA NJOMBE MJINI BI.LILIAN NYEMELE AKIZUNGUMZA KWA MASIKITIKO BAADA YA KUPOKEA TAARIFA KWA MWALIMU MKUU WA SHULE YA MSINGI LUHUJI KUHUSU BAADHI YA WAZAZI KUTELEKEZA WATOTO WAO
MWALIMU MKUU WA SHULE YA MSINGI LUHUJI BI.GRACE MRWILLO AKIZUNGUMZA
DIWANI WA VITI MAALUMU ANJELA MWANGENI AKIMKABIDHI MWALIMU MKUU WA SHULE YA MSINGI LUHUJI GRACE MRWILLO MAHINDI NA MAHITAJI MENGINE ALIOYACHUKUA KWAAJILI YA WANAFUNZI HAO.
TAYARI WANAFUNZI WAMEKABIDHIWA CHAKULA NA SASA WANAPELEKA STOO YA SHULE
DIWANI MWANGENI AKIWA NA WAJUMBE WENGINE AMBAO AMEONGOZANA NAO KUKABIDHI MSAADA
BAADHI YA WANAFUNZI WALIOTELEKEZWA NA WAZAZI WAO WAKIHOJIANA NA MWAANDISHI WA HABARI SHULENI HAPO
Kauli hiyo imetolewa mapema leo na diwani wa viti maalumu kata ya Njombe Mjini Bi.Anjela Mwangeni wakati akikabidhi msaada wa mahindi na maharage kwaajili ya chakula cha watoto yatima na wanaoishi kwenye mazingira magumu wanaosoma shule ya msingi Luhuji.
Aidha Bi. Mwangeni amesema wazazi na Walezi wanatakiwa kutambua kuwa jukumu la kulea watoto ni la kila mmoja katika Jamii Ambapo kutokana na kukosekana kwa baadhi ya mahitaji kwa watoto hao amekabidhi msaada wa mahindi debe 11,maharage debe 1,sukari Kilo kumi na fedha tasilimu shilingi elfu thelathini na kuahidi kuwasomesha baadhi ya watoto ambao wametelekezwa na wazazi wao.
Afisa Taarafa wa Njombe Mjini B. Lilian Nyemele amesema Wenyeviti wa mitaa wanatakiwa kuchukua hatua za haraka za kuwafuatilia baadhi ya wazazi ambao wametelekeza watoto wao na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria Ikiwa ni miongoni mwa majukumu yao ya kutetea na kusaidia jamii kutatua baadhi ya changamoto zinazoikabili.
Akizungumza mbele ya Diwani huyo Mwalimu Mkuu wa shule msingi Ruhuji bi.Grace Mrwillo Amesema shule hiyo inawatoto yatima na wanaoishi kwenye mazingira magumu 45 ambapo shule inalazimika kuchukua jukumu la kuwasaidia mahitaji ikiwemo ugonjwa, chakula na mahitaji ya shule.
Bi.Mrwillo amepongeza kwa hatua iliyofanywa na wadau wa elimu akiwemo Diwani wa viti maalumu Mwangeni ambae amekabidhi msaada wa chakula wenye thamaini ya zaidi ya shilingi laki moja na hamsini na kuwashukuru baadhi ya wajumbe alioongozana nao kwa kuchangia shilingi elfu thelathini na tano kama harambee fupi ikiwa hiyo ni changamoto kwa wadau wengine kusaidia watoto hao.
Kwa upande wao wadau walioongozana na Diwani huyo akiwemo katibu wa vijana wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Njombe Himid Tweve wamesikitishwa na kitendo cha baadhi ya wazazi kuwatelekeza watoto na kuahidi kuonesha ushirikiano katika kuwafichua wazazi wenye tabia kama hizo.
Wakizungumza mara baada ya kutolewa kwa msaada huo baadhi ya wanafunzi yatima,wanaoishi kwenye mazingira magumu na waliotelekezwa na wazazi wao wamesema wanakabiliwa na tatizo la ukosefu wa chakula na mahitaji mengine muhimu jambo ambalo limewalazimu kuwaeleza walimu wa shule ili kupatiwa msaada.
No comments:
Post a Comment