Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Thursday, July 31, 2014

WATU SITA WAPOTEZA MAISHA KWA AJALI YA GARI MKOANI NJOMBE-ILEMBULA

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Ambaye ni Afisa  Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Njombe Franco Kibona Akizungumza na Vyombo Vya Habari Leo 
Na Gabriel Kilamlya Njombe

Watu Sita Wamefariki Dunia na Wengine Wawili Kujeruhiwa Katika Ajali ya Lori Liliokuwa Limebeba Magunia ya Mpunga Likitokea Wilayani Mbarali Mkoani Mbeya Kulekea Makambako Mkoani Njombe.

Wakizungumzia Ajali Hiyo Baadhi ya Mashuhuda Wamesema Imetokea Leo Majira ya Saa Kumi na Moja Alfajiri Katika Njiapanda ya Kuelekea Ilembula Baada ya Gari Hilo Liligonga Ukingo wa Daraja La Mto Halali na Kupinduka Kisha Kuwafunika Baadhi ya Watu Waliokuwa Katika Gari Hilo.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Bwana Franco Kibona Amesema Kuwa Ajali Hiyo Imetokea Kwa Gari Hilo Kutumbukia Katika Mto Halali Ambao Licha ya Kuwa na Maji Machache Lakini Ndani Yake Kuna Mawe Mengi.

Kamanda Kibona Amewataja Watu Hao Waliofariki Dunia Kuwa ni Pamoja na Dereva wa Gari Hilo Bwana Zedekia Shadrack Mkazi wa Makambako  Pamoja na Wabeba Mizigo Maarufu Kwa Jina la [MAKURI] Watano Ambao Wote Wamefariki Papo Hapo.

Aidha Amewataja Majeruhi Wawili wa Ajali Hiyo Kuwa ni Samuel Ndende Mwenye Umri wa Miaka 26 Mkazi wa Makambako Ambaye Naye ni Mbeba Mizigo na Yusuph Kabulika Mwenye Umri wa Miaka 23 Mwenyeji wa Kapunga Chimala na
Mkazi wa Makambako Ambaye Yeye Aliyekuwa Utingo wa Gari Hilo.

Amesema Kuwa Majeruhi Hao Wamelazwa Katika Hospitali ya Misheni Ilembula Ambao Mmoja Kati Yao Anayefahamika Kwa Jina la Samuel Ndende Utingo Hali Yake Inaendelea Vizuri Huku Mwenzio Hali Yake Ikiwa ni Mbaya.

Amesema Kuwa Chanzo Cha Ajali Hiyo Bado Kinaendelea Kuchunguzwa.

No comments:

Post a Comment