WA UPANDE WA KULIA NI DR. MSIGWA WA HOSPITALI YA KIBENA,WA PILI KUTOKA KULIA NI DAKTARI MKUU WA MKOA WA NJOMBE DR.SAMUEL MGEMA WA TATU KUTOKA KULIA NI KATIBU TAWALA MKOA WA NJOMBE NA WA NNE TOKA KULIA NI MKUU WA MKOA WA NJOMBE KEPTAIN MSTAAFU ASERI MSANGI WAKIWA CHUMBA CHA UPASUAJI WAKISUBIRI MAKABIDHIANO YA TAA HIZO YAFANYIKE.
HIZI NDIZO TAA ZILIZOKABIDHIWA MIKONONI MWA MKUU WA MKOA WA NJOMBE KEPTAIN MSTAAFU ASERI MSANGI KWAAJILI YA HOSPITALI YA MKOA YA KIBENA NJOMBE
WATUMISHI WA AFYA WAKISHUHUDIA MAKABIDHIANO KATI YA SHIRIKA LA TAIFA LA HIFADHI YA JAMII MKOA WA NJOMBE LIKIKABIDHI TAA MBILI ZA KISASA KWAAJILI YA CHUMBA CHA UPASUAJI
WA KATIKAKATI NI MENEJA NSSF MKOA WA NJOMBE GODWIN MWAKALUKWA AKIWA CHUMBA CHA UPASUAJI KIBENA AKIKABIDHI TAA HIZO
HAWA NI WATUMISHI WA AFYA KATIKA HOSPITALI YA MKOA WA NJOMBE YA KIBENA WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA MKUU WA MKOA WA NJOMBE
MKUU WA MKOA WA NJOMBE KEPTAIN MSTAAFU ASERI MSANGI AKIHOJINA NA WAANDISHI WA HABARI BAADA YA KUKABIDHIWA TAA HIZO ZA UMEME
MENEJA WA SHIRIKA LA TAIFA LA HIFADHI YA JAMII MKOA WA NJOMBE GODWIN MWAKALUKWA AKIWA HOSPITALI YA KIBENA
HAYA NI MAGARI YA MKOA WA NJOMBE
Na Michael Ngilangwa.
Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii Mkoa wa Njombe jana limekadhi msaada wa Taa mbili za kisasa kwaajili ya chumba cha Upasuaji katika Hospitali ya Mkoa wa Njombe Kibena wenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 11.
Akikabidhi msaada huo Meneja wa Shirika la Taifa La hifadhi ya Jamii Mkoa wa Njombe NSSF Godwin Mwakalukwa amesema kuwa hatua ya kukabidhi misaada hiyo ni Muendelezo wa shirika hilo kukabidhi vifaa na mahitaji mbalimbali ambapo mpaka sasa tayari limekwisha kabidhi mashuka katika hospitali ya DDH Lugalawa na kompyuta moja kwa jeshi la Polisi mkoa wa Njombe vyenye jumla ya shilingi milioni moja na laki saba.
Aidha Bwana Mwakalukwa amesema kuwa shirika hilo pia limefanikiwa kukopesha mikopo kwa baadhi ya SACCOS saba za kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Wanging'ombe,Wilaya ya Njombe ,Makambako na Saccos ya Wafanyabiashara ya Njombe mjini yenye thamani ya shilingi bilioni moja na milioni mia nne themanini na tano ili kuinua uchumi wa wanachama wake.
Hata hivyo Bwana Mwakalukwa ametumia Fursa hiyo kuwaomba wadau wengine wa maendeleo yakiwemo mashirika na taasisi mbalimbali kujitokeza kuwasaidia misaada kwenye hospitali hiyo hususani kwenye chumba cha maiti cha Kisasa ambacho hakipo katika hospitali hiyo kongwe.
Akipokea Msaada huo kutoka kwa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii Mkuu wa Mkoa wa Njombe Keptain Mstaafu Aseri Msangi ameshukuru kwa jitihada zilizofanywa na shirika hilo kufanikisha zoezi la kuwapatia msaada wa taa za kisasa kwaajili ya chumba cha Upasuaji na kwamba limewapunguzia gharama ambazo serikali ingeanza kufikiria kuzinunua jambo ambalo lingechukua muda mrefu kununuliwa.
Aidha Keptain Msangi Ametumia nafasi hiyo kuwaomba wadau wengine kujitokeza kujenga Chumba cha kuhifadhia Maiti cha Kisasa katika Hospitali hiyo ili maiti ziweze kuhifadhiwa hapo na kwamba Chumba hicho kinaweza kuwekwa kama sehemu ya biashara kwa kutoza pesa kidogo kila nmaiti itakayopelekwa hapo.
Kwa upande wake Daktari mkuu wa Mkoa wa Njombe Dr. Samuel Mgema amesema serikali bado inaendelea na jitihada mbalimbali za kutafuta wafadhili na wadau wa kuisadia hospitali ya mkoa wa Njombe ya Kibena ili kutatua baadhi ya changamoto zinazoikabili huku serikali ikitarajia kutenga kiasi cha fedha katika bajeti ya mwaka wa fedha wa 2014/2015 kurekebisha baadhi ya miundombinu ya hospitali hiyo.
No comments:
Post a Comment