Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Wednesday, June 4, 2014

WANANCHI WA KIJIJI CHA MATIGANJORA WALAANI UCHOMAJI MOTO MAZINGIRA


 AFISA MTENDAJI WA KIJIJI CHA MATIGANJORA SAMSON NYAGAWA AKITOLEA UFAFANUZI KUHUSIANA NA FAINI YA ATAKAEKAMATWA AMECHOMA MOTO MAZINGIRA


 WANANCHI WA KIJIJI CHA MATIGANJORA WAKIWA KWENYE MKUTANO WA HADHARA KIJIJINI HAPO



 MENEJA WA KAMPUNI YA TANWAT ESTATE NO.ONE NA NO. TWO KIMASA SHEJA AKITOLEA UFAFANUZI JUU YA MATUKIO YA MOTO NA WIZI WA MAGOGO YA MITI KWAAJILI YA MBAO



 MENEJA TANWAT KIMASA SHEJA AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA MATIGANJORA

 MWENYEKITI WA KIJIJI CHA MATIGANJORA BWANA RAZARO  MWINAMI  AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WAKE KIJIJINI HAPO HUKU MTENDAJI WA KATA JOB FUTE AKITETA NA MENEJA WA TANWAT WA MASHAMBA YA NAMBA ONE NA TWO

 AFISA MTENDAJI WA KATA  YA IKUNA JOBU FUTE AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA KIJIJI CHA MATIGANJORA KUHUSIANA NA MAHUSIANO NA KAMPUNI YA TANWAT
 MTENDAJI WA KIJIJI CHA MATIGANJORA   SAMSONI NYAGAWA  KWA MSISITIZO ANAKAZIA HOJA YA FAINI YA SHILINGI LAKI TATU KWA MSABABISHAJI WA MOTO KICHAA
KIMASA SHEJA  ANAAHIDI WANANCHI WA KIJIJI CHA MATIGANJORA KUWAPATIA MAGOGO YA KUTENGENEZEA MADAWATI LAKINI MTENDAJI AANDIKE BARUA NDIPO WAPATIE MSITU WA KUKATA MAGOGO HAYO.

Wananchi wa kijiji cha Matiganjora Wilayani Njombe wamekubaliana kuanza zoezi la ujenzi wa vyoo bora na vya kisasa katika kijiji hicho  ili kuepukana na mlipuko wa magonjwa mbalimbali ambao unaweza kujitokeza kutokana na baadhi yao kuishi pasipo kujenga vyoo  vya kisasa huku wengine  wakiishi bila kujenga vyoo hivyo jambo linaloweza kusababisha madhara kwa wakazi hao.

Miongoni mwa agenda zilizojadiliwa kwenye mkutano  wa hadhara ni pamoja na wananchi kuacha tabia ya kuchoma moto ovyo,utunzaji wa mazingira na kujenga vyoo bora,kuimarisha ulinzi na usalama wa raia na mali zao ikiwemo kuwataja waharifu wanaohusika na wizi wa miti ya mbao katika msitu wa kampuni ya Tanwat pamoja na kutengeneza madawati.

Wakizungumza kwenye mkutano wa hadhara wananchi wa kijiji cha Matiganjora wamesema kuwa uwepo wa matukio ya uchomaji misitu moto holela umesababisha kurudisha jitihada za wananchi za kupanda miti na kutaka hatua kali zichukuliwe dhidi ya watakao sababisha kutokea kwa matukio ya Moto.

Akizungumza mbele ya wananchi wa kijiji hicho  afisa mtendaji wa kata ya Ikuna bwana Job Fute amekemea mvikali tabia ya uchomaji hovyo wa moto kwenye mazingira na kuwataka kubuni mbinu mbadala ya kuhakikisha matukio hayo hayatokee katika kijiji hicho ambapo pamoja na mambo mengine pia ametaka agenda ya usafi wa mazingira na kujenga vyoo vya kisasa pamoja na kutengeneza madawati kuzingatiwa kwa kila kijiji.

Akizungumza kwa upande wake Meneja wa mashamba ya miti kutoka kampuni ya Tanwat bwana Kimasa Shija amewapongeza wananchi kwa kuridhia kuimarisha ulinzi katika uchomaji wa misitu ovyo pamoja na wizi wa miti ya mbao kwenye misitu ta kampuni hiyo ambapo ameahidi kuwa karibu nao katika kuwasaidia kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali ya zahanati,shule,makanisa na utengenezaji wa madawati.

Kwa upande wao viongozi wa kijiji cha Matiganjora  mwenyekiti na afisa mtendaji wa kijiji hicho bwana Razaro Mwinami na Samson Nyagawa wameishukuru kampuni ya Tanwat kwa kuahidi kuwa karibu nao kuwasaidia kuwapatia miti kwaajili ya kutengeneza madawati ambapo pamoja na mambo mengine wameahidi kushikamana na wananchi na uongozi wa kampuni hiyo ili kutokomeza uharifu mbalimbali ambao umekuwa ukitokea.

No comments:

Post a Comment