Mitaa mbali mbali ya Ilala usafi ukifanywa na wananchi kuunga mkono siku ya uhuru wa vyombo vya habari leo
Na Diana Bisangao ,Iringa
KWA HISANI YA FRANCIS GODWIN IRINGA
WANAHABARI
mkoa wa Iringa waungana na wakazi wa kata ya Ilala katika
Halmashauri ya Manispaa ya Iringa waadhimisha siku ya uhuru wa vyombo
vya habari duniani kwa kufanya usafiri wa mazingira katika kata
hiyo ya Ilala inayoongozwa na naibu meya wa Halmashauri ya Manispaa
ya Iringa Grevas Ndaki.
Mbali
ya wanahabari hao kushiriki kuzoa taka katika eneo hilo la Ilala
pia wamefikisha neema kwa wananchi hao wa Ilala baada ya kuwaombea
chombo maalum cha kuhifadhia taka (DAMPO) ambacho walikuwa hawana na
kulazimika kutupa katakata katika kiwanja cha mkazi mmoja wa eneo hilo.
Wakizungumzia
utaratibu huo wa wanahabari Iringa kujitolea kufanya usafi wa
mazingira baadhi ya wananchi wa kata hiyo ya Ilala walisema kuwa
kilichofanywa na wanahabari hao ni mfano wa kuigwa na kuwa kwani ni
kwa mara ya kwanza katika kata hiyo wanashuhudia wanahabari hao
wakionyesha mfano wa kushika vifaa vya usafi na kuzoa taka badala ya
kuandika pekee.
Alisema
Amina Sanga kuwa baada ya kusikia katika vyombo vya habari jana
kuwa wanahabari hao wangefika kufanya usafi katika eneo lao
wengi wao walikuwa na hamu ya kushuhudia kama ni kweli wanahabari
hao watafika kufanya usafi ila baada ya kuwaona wao kama
wananchi walifarijika zaidi .
Huku
kwa upande wake Husein Ally alisema kuwa changamoto kubwa ya
usafi katika eneo hilo ni kukosekana kwa chombo cha kuhifadhia taka
na hivyo kuwafanya wananchi kutupa takataka eneo la uwanja wa mtu
jambo ambalo kiafya ni hatari zaidi kwani wapo baadhi ya watoto
wamekuwa wakishinda katika takataka hizo kuokota uchafu huo na
kuchezea.
Hivyo
waliomba wanahabari hao kuwasaidia kuwaombea chombo cha
kuhifadhia takataka ili kiweke eneo hilo na kila kinapojaa basi gari
la kubeba uchafu la Manispaa kufika na kuziondoa mapema.
Katibu
mtendaji wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IPC) Bw
Francis Godwin alisema kuwa kitaifa maadhimisho hayo yamefanyika
mkoani Arusha ambapo mwenyekiti wake Frank Leonard amekwenda
kuwawakilisha wanahabari wa mkoa wa Iringa ambapo kauli mbinu kwa
mwaka huu kitaifa ni Uhuru wa Habari kwa maendeleo na utawala bora .
Godwin
alisema kuwa mbali ya kauli mbinu hiyo ya kitaifa mkoa wa Iringa
umeongeza kauli mbinu ya pili kwa ajili ya mkoa huo mbali ya ile ya
Taifa pia wamejiongezea ile ya uhuru wa vyombo vya habari na usafi wa
mazingira ni jukumu letu sote .
Hivyo
alisema kuwa kutokana na heshima kubwa ya mkoa wa Iringa iliyopata
kupitia Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kwa kuwa ya pili kiusafi
kitaifa wao wameamua kuunga mkono jitihada hizo kwa kuhamasisha jamii
kufanya usafi katika mji huo .
Pia
kujitolea misaada mbali mbali kwa kituo cha Yatima cha DBL Mkimbizi
na kuwa suala hilo la usafi katika kata ya Ilala limefanyika kama
sehemu ya kuihamasisha jamii kuendelea kufanya usafi katika maeneo
yao .
Aidha
aliomba uongozi wa Manispaa kuunga mkono jitihada hizo kwa kuweka
Dampo eneo hilo la Ilala ili kuwawezesha wananchi hao kuwa na sehemu ya
kuhifadhi takataka.
Afisa
msimamizi wa wahudumu wa usafi katika Halmashauri ya Manispaa ya
Iringa Aron Mafumiko mbali ya kuwapongeza wanahabari hao kufika
kufanya usafi pia alikubali kuweka dampo la kudumu eneo hilo la Ilala
kama sehemu ya kuunga mkono jitihada za wanahabari hao mkoa wa Iringa.
|
No comments:
Post a Comment