Tuesday, May 6, 2014
VIONGOZI WA SACCOS HALMASHAURI YA MJI NJOMBE WANOLEWA KWA SIKU TATU
ALIYESIMAMA UKUTANA NAE NI MUWEZESHAJI AMBAE PIA NI AFISA USHIRIKA HALMASHAURI YA MJI WA NJOMBE LAWI DUWANGE
MUWEZESHAJI WA MAFUNZO ANTHELMUS TARIMO
WA KWANZA KUTOKA UPANDE WA KULIA NI MWENYEKITI WA MAFUNZO HAYO,JOSEPH MWALUWANDA,WA PILI TOKA KULIA NI MGENI RASMI ERNEST NGAPONDA WA TATU NI AFISA USHIRIKA HALMASHAURI YA MJI WILLIAM KINYAGA
AFISA USHIRIIKA HALMASHAURI YA MJI WA NJOMBE WILLUIAM KINYAGA AKITOA NASAHA KIDOGO MBELE YA MGENI RASMI
MWENYEKITI WA SACCOS YA WAFANYABIASHARA WA NJOMBE MJINI JOSEPH MWALUWANDA AKIZUNGUMZA
Halmashauri ya mji wa Njombe kwa kushirikiana na vyama vya ushirika vya akiba na mikopo SACCOS imeanza kutoa mafunzo ya siku tatu kwa viongozi 28 wa kutoka wa vyama vya ushirika vya akiba na mikopo 14 vilivyopo katika halmashauri ya mji wa Njombe ili kuwasaidia kutatua baadhi ya changamoto zinazowakabili.
Akizungumza na washiriki wa vyama vya ushirika vya akiba na mikopo ishirini na nane wakati wa kufungua semina hiyo afisa kilimo,umwagiliaji na ushirika bwana Ernest Ngaponda amewataka viongozi wa Vyama hivyo kufuata taratibu za utoaji wa mikopo pasipo kutoa kwa upendeleo kwani kumekuwa na malalamiko mengi toka kwa wateja ya kutolewa kwa upendeleo kwa mikopo katika SACCOS hiZO.
Aidha bwana Ngaponda amesema kuwa viongozi hao wanatakiwa kuwa makini na utoaji wa mikopo kwa wanachama wake huku mameneja wakitakiwa kusimamia kwa umakini SACCOS hizo ili kuleta manufaa kwa wanachama wake na kwamba Serikali inatambua uwepo wa vyama hivyo jambo ambalo linapelekea kila halmashauri kutenga bajeti kwaajili ya vyama hivyo kukopesha wananchi.
Amesema kuwa halmashauri inajukumu la kuwasaidia wanachama wa SACCOS kwa kutoa mafunzo mbalimbali pamoja na kutoa fedha kupitia idara ya Ushirika ili vyama hivyo viweze kujiendesha na kumudu matakwa ya wanachama wake.
Awali akimkaribisha Mgeni rasmi makamu mwenyekiti wa Chama cha ushirika cha wafanyabiashara wa Njombe mjini ambae pia ni mwenyekiti wa semina hiyo bwana Joseph Mwaluwanda amesema kuwa semina hiyo imewashirikisha viongozi wa vyama vya akiba na mikopo wakiwemo wenyeviti na mameneja wa kutoka SACCOS 14 za halmashauri ya mji wa Njombe.
Kwa upande wao washiriki wa semina hiyo wakichangia hoja mbalimbali pamoja na kuishukuru halmashauri kwa kuunga mkono uwepo wa vyama hivyo wametaka wataalamu wa mifuko ya hifadhi ya taifa ya jamii kuwafikia ili wanachama wa vyama hivyo waweze kujiunga huku wanachama wakishauriwa kujiunga kwenye vyama vya wafanyakazi na kutetea haki zao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment