Thursday, May 29, 2014
KIJIJI CHA MANGALANYENE WILAYA YA LUDEWA CHAKABILIWA NA UHARIBIFU WA MIUNDOMBINU YA BARABARA PAMOJA NA MIGOGORO YA ARDHI
Wananchi wa kijiji cha Mangaranyene kata ya Madope Wilayani Ludewa wamelalamikia kuwepo kwa ubovu wa miundo mbinu ya barabara na kwamba wanashindwa kusafirisha mazao na kusafiri kuelekea Njombe na wilayani Ludewa kutokana na magari kushindwa kupita kwa wakati kwaajili ya Uharibifu huo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi hao wameomba serikali wilayani Ludewa kuilima barabara hiyo katika msimu huu ambao mvua zimepungua ili kurahisisha huduma ya usafiri kwa wakulima na wananchi wa kata za Madope na Madilu na kwamba kuharibika kwa miundombinu hiyo kumesababisha baadhi ya akina mama wajawazito na wagonjwa kushindwa kuzifikia huduma za afya kwa urahisi.
Akizungumza Kijijini hapo Afisa Mtendaji wa kijiji cha Mangaranyene kata ya Madope Wilayani Ludewa bwana Octavian Mtewele amesema wakazi wa kijiji hicho wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kukosekana kwa zahanati ya kijiji jambo linalosababisha wakazi wa eneo hilo kusafiri umbali wa takribani kilomita 8 hadi kuzifikia huduma za afya.
Aidha bwana Mtewele amesema kuwa kuharibika kwa miundombinu ya barabara ni miongoni mwa changamoto zinazowakabili wakazi wa kijiji hicho na vijiji vya kata za jirani kwa msimu wa mvua kutokana na magari kukwama na kushindwa kusafirisha abiria kwa urahisi ambapo amesema ujenzi wa zahanati ya kijiji hicho umeanza na inatarajia kugharimu zaidi ya shilingi milioni 1shirini ambayo muda wa kukamilika inategemea msaada wa vifaa vilivyoahidiwa na Mbunge wa Ludewa.
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Madope bwana Godfrey Mhagama amekili kuwepo kwa changamoto ya miundombinu ya barabara na kwamba halmashauri ya Wilaya ya Ludewa inatarajia kuboresha miundombinu hiyo mara mvua zikimalizika kunyesha na kuwaomba wananchi kuwa wavumilivu wakati tatizo hilo likitatuliwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment