WA UPANDE WA KULIA NI HAKIMU MKAZI MFAWIDHI MWANDAMIZI WA MAHAKAMA YA WILAYA YA NJOMBE AUGUSTINO RWIZILE,WA PILI NI BABA PAROKO TOKA KANISA KATHOLIKI JIMBO LA NJOMBE NA WA TATU NI ASKALI MSTAAFU WA JESHI LA POLISI AMBAE AMESTAAFU MWAKA HUU INSP. KOSMAS
HAWA NDIYO WAAGWA WA UPANDE WA KULIA NI AFISA MNADHIMU MWANDAMIZI WA JESHI LA POLISI MKOA WA NJOMBE,WA PILI KUTOKA KULIA NI R.C.O ALLAN BUKUMBI MWENYE SUTI NYEUSI,WA TATU TOKA KULIA NI SSP FRANCIS MALO,WA NNE TOKA KULIA AMEHAMIA ATAKUWA R.T.O MKOA WA NJOMBE JAMES KITELEKI NA WA TANO ANAMUWAKILISHA ALIYEKUWA R.T.O MKOA WA NJOMBE AMBAE NI MKEWE NA CHACHA MALO.
MKUU WA WILAYA YA NJOMBE BI.SARAH DUMBA AKIKABIDHI ZAWADI KWA WAAGWA
SHANGWE KUBWA SIKU YA HAFRA FUPI YA KUWAAGA WALIOHAMISHWA WATUMISHI WA JESHI LA POLISI MKOA WA NJOMBE
DESDELIA MTAMITA AKIWA NA MWENZA WAKE WA UPANDE WAKE WA KULIA ALIESHIKA GONGO LA KUTEMBELEA
MTANGAZAJI WA JAHAZI LA PWANI KATIKA RADIO UPLANDS FM MAARUFU MAMA NYEUPE JINA LAKE HALISI PILY NYENJE AKIWASHUKURU WADAU WA ULINZI NA USALAAMA WA JITIHADA WANAZOFANYA KWA NIABA YA RADIO UPLANDS
Jeshi la polisi mkoa wa Njombe jana limewaaga baadhi ya wafanyakazi wanaohamia mikoa mingine hapa nchi ambapo pamoja na mambo mengine wananchi wametakiwa kuendelea kuonesha ushirikiano kwa wale watakao kuja kubadili nafasi ya waliohama.
Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi.Sarah Dumba wakati wa hafra fupi ya kuwaaga wafanyakazi wanaohamia mikoa mingine pamoja na kumpongeza Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Njombe Fulgence Ngonyan kwa kupandishwa cheo kutoka ACP na kuingia SACP na kwamba hatua hiyo imekuja kutokana na utendaji mzuri wa kazi.
Aidha Bi.Dumba amewataka askali wanaohamia sehemu nyingine kwenda kuendeleza yale mazuri waliokuwa wakiyafanya wakiwa mkoa wa Njombe na kwamba utendaji wao wa kazi utakaokubalika na jamii ndiyo mafanikio yao Huku akiwataka waliohamia mkoa wa Njombe kuendeleza jitihada za kufanya kazi kwa weledi ili kusiwepo na dosali yoyote.
Awali akimkaribisha mgeni rasmi Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Njombe SACP Fulgence Ngonyani amewapongeza wafanyakazi wa jeshi hilo wanaohama kwa jitihada mbalimbali walizofanya wakiwa mkoa wa Njombe huku akisema hafra hiyo inakwenda sambamba na kumpongeza askali wa polisi Insp Cosmas kwa kustaafu kwake.
Kamanda Ngonya amewataja wanaohamia mikoa mingingine kuwa ni pamoja na aliekuwa Mnadhimu wa jeshi la polisi mkoa wa Njombe SSP Focus Malengo anaekwenda kuwa staafu officer namba 1 mkoa wa Katavi,SP Mshana Mjema anaekwenda kuwa OCD Mbagala,ASP Chacha Marwa anakwenda kuwa R.T.O Ilala, OCD Wilaya ya Wanging'ombe Francis Marwa anakwenda kuwa R.C.O Mkoa wa Katavi na SSP Alan Bukumbi anakwenda kuwa R.C.O Mkoa wa Rukwa huku akiwataja waliohamia mkoa wa Njombe.
Amesema kuwa kutokana na kuhamishwa kwa wafanyakazi hao pia kuna waliohamia mkoa wa Njombe kufanya kazi za kipolisi ambao ni pamoja na Mkuu wa usalama wa Barabarani R.T.O James Kiteleki na Franco Kibona ambae atakuwa mkuu wa upelelezi mkoa wa Njombe.
No comments:
Post a Comment