Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Wednesday, March 26, 2014

SIKU YA KIFUA KIKUU YAADHIMISHWA KWA WILAYA YA NJOMBE KATIKA KIJIJI CHA LWANGU


WANANCHI WA KIJIJI CHA LWANGU WAKIWA KWENYE KWAYA  WAKIBURUDISHA UMATI WA WAKAZI WA KIJIJI HICHO






MKUU WA WILAYA YA NJOMBE AKIWA NA WAGENI WENGINE AKIELEKEA KWENYE MABANDA YA MAONESHO KUKAGUA



MKUU WA WILAYA YA NJOMBE AKIPIMWA KATIKA MABANDA YA MAONESHO KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA KIFUA KIKUU ILIYOFANYIKIA KIWILAYA KATIKA KIJIJI CHA LWANGU MNAMO TAREHE 24 MACH 2014.


WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI LWANGU WAKIWA KWENYE KWAYA YA SHULE WAKIIMBA MBELE YA MGENI RASMI AMBAE NI MKUU WA WILAYA YA NJOMBE .



MKUU WA WILAYA YA NJOMBE BI.SARAH DUMBA AKITOA ZAWADI KWA WALIOIMBA VIZURI SIKU YA KIFUA KIKUU MACH 24 MWAKA HUU.

Wananchi wilayani Njombe wametakiwa kujitokeza kwa wingi kwenda kupima afya zao katika hospitali na vituo vya afya vilivyo karibu nao ambapo pamoja na mambo mengine wanatakiwa kuondokana na Imani potofu za kwenda kwa waganga wa jadi badala yake waende katika hospitali na vituo vya afya kupimwa na kutibiwa haraka.

Akiongea na wananchi wa kijiji cha Lwangu katika kilele cha siku ya kifua kikuu mkuu wa Wilaya ya Njombe bi. Sarah Dumba amesema kuwa serikali wilayani Njombe inaendelea na jitihada za kuongeza vituo vya afya vya kutolea huduma za matibabu ya ugonjwa wa Kifua kikuu  na kufanikiwa kutibiwa kwa wakati.

Aidha Bi.Dumba amesema kuwa wananchi wanatakiwa kutambua kuwa Kifua kikuu ni ugonjwa hatari kwani umechangia kwa kiasi kikubwa kusababisha vifo vingi vya wananchi ambapo amesema ugonjwa huo unatribika huku wakishauriwa kuepukana na mikusanyiko ya watu,kutema ovya makohozi,kuishi kwenye nyumba zenye mizunguko ya hewa na mwanga wa kutosha na kuwagundua watu wenye ugonjwa huo na kuwapeleka hospitali kutibiwa.

Amesema kuwa kifua kikuu ni Ugonjwa unaoambukizwa kwa njia ya hewa ambapo njia nyingine moja wapo ya kuzuia maambukizi ya Ugonjwa huo ni pamoja na kuwachanja chanjo watoto kinga ya kifua kikuu pamoja na kutoa risha ya kutosha hivyo chakula bora kinatakiwa kutolewa sehemu zote shuleni na nyumbani Huku akizitaja dalili za kifua kikuu kama anavyo eleza.

Akisoma Taarifa fupi kwa Mkuu wa Wilaya ya Njombe Mratibu wa Kifua kikuu Wa halmashauri ya Mji wa Njombe bwana Leo Chrispo Chaula amesema kuwa halmashauri ya mji ina jumla ya vituo vya kutolea huduma za afya hamsini na tano ambapo kati ya hivyo, vituo hamsini na moja hutoa dawa kwa wagonjwa wa kifua kikuu chini ya muhudumu wa afya ngazi ya jamii katika vituo hivyo 55.

Maadhimisho ya Kifua kikuu kwa Halmashauri ya Wilaya na Mji yamefanyikia kijiji cha Lwango yakiwa na Kauli mbiu isemayo FIKIA KILA MTU,GUNDUA,TIBU NA PONYA MGONJWA WA TB ambapo hii inafanyika ili kuwakumbusha na kuwaelimisha wananchi kuhusu Kifua kikuu,Matibabu,mahusiano kati ya Kifua kikuu na UKIMWI na namna ya kuzuia maambukizi ya Kifua kikuu  na kuwahamasisha wadau ili kuweka mikakati ya kudhibiti Kifua kikuu.

No comments:

Post a Comment