Thursday, February 27, 2014
MKUU WILAYA YA NJOMBE AHIMIZA TOHARA KWA WANAUME KIJIJI CHA NYOMBO LEO
MKUU WA WILAYA YA NJOMBE BAADA YA KUWASILI KATIKA UWANJA WA MKUTANO KATA YA IKUNA
AFISA MTENDAJI WA KATA YA IKUNA BWANA JOBU FUTE AKITAMBURISHA WAGENI WALIOKUWEPO
WA UPANDE WA KULIA NI DIWANI WA KATA YA IKUNA VALENTINO HONGORI,ANAEFUATIA KWAKE NI MWENYEKITI WA KIJIJI CHA NYOMBO BWANA LISULILE,ANAEFUATIA NI MKUU WA WILAYA YA NJOMBE BI SARAH DUMBA NA WA MWISHO NI KATIBU TAWALA WILAYA YA NJOMBE.
DIWANI WA KATA YA IKUNA BWANA VALENTINO HONGORI AKITOA NASAHA KWA WANANCHI
AFISA TAARAFA YA MAKAMBAKO AKIWA NA AFISA MTENDAJI WA KATA YA IKUNA
MKUU WA WILAYA YA NJOMBE BI SARAH DUMBA AKITOA HOTUBA YAKE KWA WANANCHI WA KIJIJI CHA NYOMBO WILAYANI NJOMBE
ASKARI WA MGAMBO WAKIWA KATIKA MKUTANO HUO KUIMARISHA ULINZI NA USALAMA
HAWA NI WANANCHI WA KIJIJI CHA NYOMBO WAKIWA MAKINI KUSIKILIZA HOTUBA YA MKUU WA WILAYA YA NJOMBE
Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi. Sara Dumba Amewashauri Wanaume Wilayani Hapa Kujitokeza
Kwa Wingi Kufanyiwa Tohara Inayoendelea Mkoani Njombe Kwa Lengo la Kupunguza Kasi ya
Maambukizi Mapya ya Virusi Vya Ukimwi.
Bi. Dumba Ametoa Rai Hiyo Hii Leo Wakati Akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Nyombo
Ambapo Amewataka Wanawake Kuwahimiza Waume Zao Kufanyiwa Tohara Ambayo Itawasaidia
Kinamama Kutoambukizwa Magonjwa ya Zinaa Pamoja na Magonjwa ya Kansa .
Aidha Mkuu Huyo wa Wilaya Amewataka Viongozi wa Ngazi za Vijiji , Kata Pamoja na Walimu
Kuwaelimisha Wananchi na Wanafunzi Wao Juu ya Umuhimu wa Tohara Pasipo Kuathiri Imani na
Masomo Yao.
Valentino Hongori ni Diwani wa Kata ya Ikuna Ambaye Amemuhakikishia Mkuu wa Wilaya Huyo
Kuwa Uongozi wa Kata Hiyo Kwa Kushirikiana na Wataalam wa Afya Wataendelea Kuwaelimisha
Wanaume na Vijana Juu ya Umuhimu wa Kufanyiwa Tohara Kupitia Vikao na Mikutano Yao ya
Hadhara.
Kwa Upande Wao Baadhi ya Wanawake Wamesema Licha ya Changamoto wanazokutana Nazo
Wataendelea Kuwahimiza Waume na Vijana Wao , Huku Wanaume na Vijana Nao Wakisema
Pamoja na Changamoto Kadhaa Zinazojitokeza Katika Kampeni Hiyo Wameahidi Kujitokeza
Kwenye Vituo Vinavyotolea Huduma Hiyo Ili Wapatiwe Huduma ya Tohara
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment