Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Saturday, February 1, 2014

BWENI LA SHULE YA SEKONDARI YA WAVULANA NJOMBE {NJOSS} LA TEKETEA KWA MOTO NA MALI MBALIMBALI ZA WANAFUNZI JIONI LEO MJINI NJOMBE




 Kikosi cha Zima Moto na Uokoaji Mkoa wa Njombe Kimepongezwa Kwa Kuwahi Kufika Eneo la Tukio na Kufanikisha Kuzima Moto Huo
 Wanafunzi Wakihamisha Baadhi ya Vitu Vilivyookolewa Katika Bweni Hilo
 Kiongozi wa Bweni Hilo Akizungumzia Jinsi Moto Ulivyotokea






Katika Hali Isiyo ya Kawaida Moto Mkubwa Umeunguza Bweni la Wanafunzi Katika Shule Ya Sekondari Njombe [NJOSS] na Kuteketeza Vitu Mbalimbali Vya Wanafunzi Hao Jioni ya Leo.

Tukio Hilo Limetokea  Majira ya Saa Kumi na Mbili Jioni Ambapo  Vitu Mbalimbali Ambavyo ni Vifaa Vya Masomo Kwa Wanafunzi Hao Vimeteketea Kwa Moto Huo.

Wakizungumza na mtandao huu Katika Eneo la Tukio Baadhi yha Wanafunzi wa Shule Hiyo Wamesema Bado Hawajatambua Chanzo cha Moto Huo Japo Kwa

Taarifa za Awali Zinaeleza Kuwa ni Shoti ya Umeme.

Akizungumzia Tukio Hilo Kiongozi wa Bweni Katika Shule Hiyo ya Wavulana  Amesema Kuwa Moto Huo Umetokea Wakati Wanafunzi Wakiwa Ukumbini Kuangali Mpira Kwenye Luninga.

Akizungumzia Tukio Hilo Diwani wa Kata ya Mjimwema Bwana Jimy Ngumbuke

Amesema Kuwa Pamoja na Kutokea Kwa Athari Kubwa Kwa Wanafunzi Hao
Lakini

Hakuna Mwanafunzi Aliyejeruhiwa Wala Kupoteza Maisha.

Bwana Ngumbuke Pia Amepongeza Kikosi cha Zima Moto na Uokoaji Mkoa wa

Njombe Kwa Kuwahi Kufika Katika Eneo la Tukio na Kufanikiwa Kuzima Moto Huo

Licha ya Kuunguza Baadhi ya Mali za Wanafunzi.


Bado Thamani Halisi ya Hasara Iliyotokea Kufuatia Kutokea Kwa Moto Huo Huku

Serikali Ikiahidi Kuendelea Kutoa Taarifa Zaidi ya Hali ya Tukio Hilo.

No comments:

Post a Comment