Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Friday, January 31, 2014

KUJAA KWA VYOO KATIKA KILABU CHA AKINA MAMA CHA TUPENDANE CHA SABABISHA KUFUNGWA KWA KILABU HICHO




 HIKI NI CHOO CHA WAFANYABIASHARA WA KILABU CHA POMBE ZA KIENYEJI CHA NJOMBE MJINI AMBACHO KINAJAA KILA SIKU NA AKINA MAMA HUCHOTA KWA NDOO ZA RITA KUMI NA KUMWAGA KWENYE SHIMO KUBWA LA HAPO WANAPOTOKEA AKINA MAMA HAO.
 HIKI NI CHOO KIPYA KINACHOJENGWA LAKINI KWA SASA KIMESIMAMA KUTOKANA NA SABABU AMBAZO HAZIKUFAHAMIKA.



 HILI NI DAMBO AMBALO LIPO USONI MWA KILABU CHA WAFANYABIASHARA HAO


 HAYA NI MAENEO YA KILABU CHA POMBE ZA KYENYEJI CHA NJOMBE MJINI KINACHOMILIKIWA NA SERIKALI.

Siku Chache Toka Uplands Redio Kuripoti Juu ya Huduma Mbovu za Vyoo Katika Kilabu cha Pombe za Kienyeji cha Tupendane Mjini Njombe,Uongozi wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Kwa Kushirikiana na Idara ya Afya Imekifungia Kilabu Hicho Hadi Hapo Huduma za Vyoo Zitakapoboreshwa.

Hatua Hiyo Pia Imekuja Kufuatia Malalamiko Yaliyotolewa na Baadhi ya  Wafanyabiashara wa Kilabu Hicho Wakidai Kuwa Vyoo Hivyo Vimeharibika na Kujaa Hali Inayosababisha Kuhatarisha Maisha na Afya ya Wakazi wa Maeneo Hayo na Wafanyabiashara Hao.

Akizungumzia Ujenzi wa Choo Katika Kilabu Hicho Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Edwin Mwanzinga Amesema Amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Kuhakikisha Anatoa Fedha Ili Kukamilisha Ujenzi Huo, Kama Anavyoeleza.

Hata Hivyo Mwenyekiti Huyo Amesema Kwa Mujibu wa Mkataba Mkandarasi Aliyepewa Kujenga Choo Hicho Kampuni ya K-9 Alitakiwa Awe Amekamilisha Ujenzi Huo Juni 2013 Lakini Hadi Sasa Ameshindwa Kukamilisha Kutokana na Uhaba wa Fedha .

Januari 29 Mwaka Huu Uplands Redio Ili Ripoti Juu ya Huduma Mbovu za Vyoo na Hali ya Usafi wa Mazingira Katika Kilabu cha Pombe za Kienyeji cha Tupendane , Jambo Lililopelekea Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Kumuagiza Afisa Afya Kufunga Kilabu Hicho.

No comments:

Post a Comment