MAMA ASHA BILAL MGENI RASMI TUZO ZA MWANAMAKUKA KATIKA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI
Mke
wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal,
akiwahutubia wanawake na wageni waalikwa katika hafla ya utoaji wa Tuzo za
Mwanamakuka 2013, zilizofanyika sambamba na uksherehekea siku ya
Wanawake Duniani, katika Ukumbi wa Hoteli ya Serena jijini Dar es
Salaam, jana Machi 8, 2013. Picha na OMR
Mke
wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed
Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi ya hundi ya Sh. milioni 6, mshindi wa
kwanza wa
Tuzo za Mwanamakuka 2013, Aziza Mbogolume, wakati wa hafla ya utoaji
tuzo hizo iliyofanyika sambamba na kusherehekea siku ya Wanawake
Duniani, katika Ukumbi wa Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Picha na OMR
Mke
wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal,
na baadhi ya wageni waalikwa wakishiriki kucheza muziki na msanii wa
muziki wa
kizazi kipya, Baby Husna, wakati akitoa burudani kwenye hafla ya kutoa
tuzo za Mwanamakuka 2013 zilizofanyika sambamba na sherehe za siku ya
Wanawake Duniani, katika ukumbi wa Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam jana Machi 8, 2013. Picha na OMR
Washiriki
wa onyesho la mitindo ya mavazi ya Mwanamakuka, wakipita jukwaani
wakati wa hafla hiyo ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa Tuzo za Mwanamakuka
2013, ambapo zawadi hizo zilikabidhiwa na Mke wa Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, jana Machi 8, 2013
katika ukumbi wa Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Picha na OMR
No comments:
Post a Comment