Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Saturday, February 23, 2013

NJOMBE STARS BAND WANAMSURI LEO NDANI YA UKUMBI WA OVACADO CLUB.








Raha jipe mwenyewe hakika pata shika katika burudani ukumbi wa ovacado club mjini Njombe.






Mwana dada amecheza hadi anataka kudondokea kwenye maic  baada ya kuipata radha ya muziki wa live toka Njombe stars bend wanamsumari.

Bendi ya Njombe stars wana wa Msumari jana jumamosi wameendelea kutumbwiza katika ukumbi wa OVA CADO CLUB ambapo umati wa wadau wa muziki wa dansi wali miminika kutazama na kuburudika na muziki huo.

Bendi ya Njombe stars ama wanamsumari wamekuwa wakifanya maonesho ya burudani ya muziki wa dansi kwa kucharaza kila aina ya nyimbo zikiwemo za watu waliopiga zamani na za sasa ili kuwaburudisha wapenzi wake.

Meneja wa Bendi hiyo bwana Joshuwa Kibangu amesema  kwa sasa bendi hiyo haija pata mpinzani katika mkoa wa Njombe hivyo wanayo nafasi kubwa ya kuhakikisha wanajiandaa na kutoa burudani ya kutosha kwa wapenzi wake wa muziki wa Danzi kam a unavyoona hapo juu.

Muziki wa dansi unaopigwa na bendi ya Njombe stars wanamsuri umewateka wazee kwa vijana wakiwemo akina mama na akina dada wote wakikusanyika katika ukumbi wa ova cado kushuhudia vijana wa Njombe  stars wanamsumari wanavyofanya mambo makumbwa ndani ya ukumbi huo.

Pamoja na hayo meneja wa Bendi hiyo bwana Kibangu alisema kuanzia mwezi mach mwaka huu wanatarajia kurecord wimbo mmoja uliotungwa na bendi hiyo ikiwa hadi sasa wanacheza nyimbo za kuiga lakini kwa sasa wanataka kurecord ili kuona kama wanawapenzi katika kszi hiyo ya muziki.

Ndugu msomaji endelea kufuatilia habari za bendi hii tutakuja kukujuza historia ya bendi hii ilikotokea na mwanzo wake ulikuwaje.

picha na Michael Ngilangwa-- Njombe.

No comments:

Post a Comment