Zao la viazi Mviringo latajwa kuwa chanzo cha mauaji msimu wa mavuno kwa wananchi wa kijiji cha Iwungilo mkoani Njombe.
Mama na mwanae amesema mume wake wanaogopa kufanya kazi za kilimo kwa hofu ya kuuwawa na majambazi.
Huyu ni mwananchi wa kijiji Iwungilo akidai ndugu zake watatu wameuwawa na majambazi mara tu walipo uza viazi lakini watuhumiwa walipokamatwa wamekaa miezi tisa wamerudi kijijini na kuwatishia tena.
Brasius Mguli akilalamika kwamba mnamo tarehe 12 december 2012 kaka
yake aliuwawa kwa risasi na majambazi cha kushangaza watuhumiwa
walipofikishwa polisi waliachiwa kwa dhamaana.
Diwani kata ya Iwungilo Musa Mlowe akimkaribisha OCD asikilize kero za wananchi za mauaji ya kutumia silaha.
OCD Njombe akisikiliza malalamiko ya wananchi wa kijiji cha Iwungilo.
Wananchi wa Kijiji Cha Iwungilo Tarafa ya Igominyi Wilayani Njombe Wamelilalamikia Jeshi la Polisi Wilayani Humo Kwa Kushindwa Kuchukua Hatua Dhidi ya Matukio ya Mauaji Yanayotokea Mara Kwa Mara Katika Kijiji Hicho.
Aidha Wananchi Hao Pia Wamelituhumu Jeshi Hilo Kujihusisha na Vitendo Vya Rushwa Kutokana na Kuwaachia Watuhumiwa Wanaofikishwa Kwao Bila ya Kuwafikisha Mahakamani Kwa Ajili ya Kusomewa Mashtaka na Kuchukuliwa Hatua za Kisheria.
Wakizungumza Mbele ya Kamanda wa Polisi Wilaya ya Njombe Wakati wa Mkutano Uliofanyika Kijijini Humo,Wananchi Hao Wameshangazwa na Kitendo Cha Jeshi Hilo Kushindwa Kuchukua Hatua Zozote Licha ya Kupewa Taarifa Juu ya Matukio Zaidi ya 12 ya Mauaji ya Kutumia Silaha Yaliotokea Kwenye Kijiji Hicho.
Pamoja na hayo wananchi hao wamesema hawana uhakiki na usalama wa maisha yao kwani matukio ya mauaji yanatokana na utajiri wa kilimo cha viazi kinachoendelea kijijini humo kwani wanaouwawa wakati wa mavuno ya viazi na kuvunjiwa nyumba zao.
Pia wameomba kujengwa kwa kituo cha polisi katika kijiji cha Uwemba ambako ni jirani na vijiji vingine vya taraafa hiyo nakusema kuwa huenda matukio hayo yanatokana na kuwepo kwa umbali wa kufuata kituo cha polisi huku wakisema wamekuwa wakipoteza nauli hadi kituo cha polisi lakini hakuna msaada wowote juu ya walalamikaji kwa polisi kusimama upande wa mtuhumiwa.
Kuhusu suala la mwananchi kujaza mafuta kwenye gari la polisi Njombe nalo likawa ni miongoni mwa mijadala na maswali yaliyoulizwa na wananchi hao kwa OCD Mwakafwila na kusema endapo kuna tukio kama mwananchi hana pesa ya kujaza mafuta hakuna msaada utakaopatikana toka kituo cha polisi.
Akizungumza Kwenye Mkutano Huo Kamanda wa Polisi Wilaya ya Njombe Lucy Mwakafwila Amewataka Wananchi Hao Kujihepusha na Vitendo Vya Rushwa Huku Akiahidi Kuyafanyia Kazi Malalamiko Yote Yaliotolewa na Wananchi Hao.
Aidha kuhusu suala la kujaza mafuta kwenye gari hali inayopelekea kushindwa kufikisha matukio yote ya uharifu pamoja na watuhumiwa kuachiwa huru pasipo mlalamikaji kufahamu.
Awali Akizungumza Kwenye Mkutano Huo Diwani wa Kata ya Iwungilo Bwana Musa Mlowe Alisema Lengo la Kumtaka Kamanda Huyo wa Polisi wa Wilaya Kufika Kijijini Hapo ni Kwa Ajili ya Kuzungumza na Wananchi na Kusikia Kero Zao Kuhusu Tatizo la Mauaji ya Kutumia Silaha Ambalo Limeanza Kutishia Usalama wa Kijiji Hicho.
Kwa Mujibu wa Wananchi wa Kijiji Cha Iwungilo,Takribani Watu 12 Wameuawa Kijijini Humo Katika Kipindi Cha Mwaka 2007 Hadi Mwaka Jana Kwa Kutumia Silaha Jambo Linalowafanya Kuhoji Uhalali wa Watu Hao Kumiliki Silaha za Moto na Wapi Wanapozipata.
No comments:
Post a Comment