Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Saturday, January 12, 2013

MAAZIMISHO YA MIAKA 49 YA MAPINDUZI YA ZABAR KWA MKOA WA NJMBE YAMEFANYIKIA HALMASHAURI YA MAKAMBAKO.

 Mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya Njombe Srah Dumba akiwasili kwenye uwanja wa sherehe  akimuwakilisha mkuu wa mkoa wa Njombe katika maadhimisho ya mapinduzi ya zanzibar kimkoa yamefanyikia Makambako Mkoani Njombe.
 
 Muungano wa vijana wa scauti kutoka shule mbalimbali za msingi na sekondari  makambako wakijiandaa kuupokea ugeni katika maadhimisho hayo.



Scuti makambako wakionesha kazi zao kwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya mapinduzi ya zanzibar.

Wanafunzi wa shule za msingi makambako wakitumbwiza mara baada ya ugeni kuwasili uwanjani.

Katibu tawala wa mkoa wa Njombe akimtamburisha mgeni rasmi na kumsimamisha atoe hotuba kwa wananchi wa makambako.



Mgeni rasmi Sarah Dumba akiwa jukwaani akitoa hotuba kwa wananchi wa makambako.

Aliyesimama mwenyekiti wa halmashauri ya makambako na mwakilishi wa madiwani wote wa halmashauri hiyo Chesco Hanana Mfikwa akishukuru kwa hotuba iliyotolewa na mgeni rasmi kwa niaba ya viongozi wote wa halmashauri.



Mkurugenzi halmashauri ya mji wa Njombe George Mkindo akitoa salamu pia awali mara tu baada ya ugeni kuwasili.



Serikali Mkoani Njombe Imekemea Vikali Tabia ya Baadhi ya Walimu wa Shule za Msingi Kuwafukuza Wanafunzi Kwa Madai ya Kukosa Ada na Hivyo Kusababisha Wanafunzi Hao Kukosa Masomo Jambo Linalosababisha Matokeo Mabaya Kwa Wanafunzi Hao Mwishoni Mwa Mwaka.

Badala Yake Serikali Imewataka Walimu Hao Kuwaruhusu Wanafunzi Kuendelea na Masomo Huku Wakifanya Mazungumzo na Wazazi Kuangalia Namna Watakavyolipa Ada Hizo Bila Kuathiri Ratiba ya Masomo Kwa Mwanafunzi Husika.





Akizungumza Kwa Niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe Wakati wa Maadhimisho ya Miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar Yaliofanyika Leo Kimkoa Mjini Makambako,Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi Sara Dumba Amesema Walimu Wanapaswa Kubuni Njia Mbadala Itakayosaidia Kupatikana Kwa Michango Hiyo Bila Kuwapa Mzigo Mkubwa Wazazi Ambao Pia Wanalazimika Kusimamia Maendeleo ya Watoto Wao Kitaaluma

Kuhusu Zoezi la Usambazaji wa Pembejeo za Ruzuku Kwa Wakulima Bi Dumba Amesema Serikali Tayari  imeanza kusambaza Pembejeo Hizo Ambazo Kwa Mwaka Huu Zimekuwa Zikisambaza na Makampuni Walioteua Mawakala Kuwafikia Wakulima.

Kwa Upande Wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Makambako Bw Chesco Hanana Mfikwa Amesema Ataendelea Kufuatilia Matatizo Mbalimbali Yalioanza Kulalamikiwa na Wazazi Tangu Kuanza Kwa Muhula Mpya wa Masomo Mwaka Huu.

Wakati Huohuo Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe Mkoani Njombe Bi.Esterina Kilasi Amemwagiza Afisa Tarafa ya Imalinyi Bwana Edward Mgaya Kuwasilisha Taarifa Zilizopelekea Baadhi ya Maafisa Watendaji na Walimu Kususia Kufika Kwenye Maadhimisho ya Miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Agizo Hilo Amelitoa Wakati wa Maadhimisho ya Miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanziba Yaliyofanyika Katika Kijiji cha Igagala Tarafa ya Imalinyi Wilayani Wanging'ombe Kwa Wilaya za Njombe na Wanging'ombe.

No comments:

Post a Comment