Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Makambako Bi.Tina Sekambo kulia pamoja na madiwani wa halmashauri hiyo wakiongozwa na mwenyekiti wao Bwana Hanana Mfikwa.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa MAKAMBAKO Mh.Chesco Hanana Mfikwa akifunga kikao cha baraza la madiwani leo.
Halmashauri ya Mji wa Makambako Wilayani Njombe Iko Kwenye Mchakato wa Kuongeza Maeneo ya Kiutawala Ili Kusogeza Huduma za Kijamii Kwa Wananchi.
Uamuzi wa Halmashauri Hiyo Umekuja Kufuatia Hali ya Jiografia ya Mji wa Makambako na Vijiji Jirani , Huku Maeneo Yaliyopendekezwa Kuwa Maeneo ya Kiutawala ni Pamoja na Kata ya Saja na Baadhi ya Vijiji Vya Kata ya Wanging'ombe.
Wakiongea Kwenye Kikao Cha Baraza la Madiwani Halmashauri ya Mji wa Makambako Wajumbe wa Baraza Hilo Wamesema Hivi Sasa Hatua Inayofuata ni Kuongea na Wananchi wa Kata na Vijiji Hivyo Jinsi ya Kuwagawa Ili Waweze Kupata Huduma Zote za Msingi.
Miongoni mwa madiwani waliochangia Agenda hiyo iliyoonekana kuwa ya pekee katika kikao hicho ni pamoja na diwani wa kata ya Kitandililo bwana John Mwandoloma ambaye alisema kuwa kwa kuwa wakazi wa kijiji cha Mtewele kilichopo kata ya Wanging'ombe na wakazi wa kata ya Saja kupata huduma katika halmashauri hiyo ni wazi kuwa wanahitajika kuingizwa kwenye halmashauri hiyo.
Kwa Upande Wake Mwenyekiti wa Halmashauri Hiyo Bwana Chesco Hanana Amesema Kwa Kuwa Madiwani wa Halmashauri Hiyo Kukubali Kuongeza Maeneo ya Kiutawala Kazi Inayofuata ni Kuwa Elimisha Wananchi Juu ya Hatua Hiyo na Kufanya Mazungumzo na Uongozi wa Wilaya ya Wanging'ombe.
Kikao cha baraza hilo katika halmashauri ya mji wa Makambako kimekuja ikiwa imepita siku moja tangu baraza kama hilo kufanyika katika halmashauri ya wilaya ya Njombe na Wanging'ombe.
No comments:
Post a Comment