Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Wednesday, July 1, 2015

WAMILIKI NA MADEREVA WATOA MAONI JUU YA ONGEZEKO LA NISHATI YA MAFUTA




Kufuatia Serikali Kupitia Mamlaka Ya Udhibiti Wa Nishati Na Maji Nchini EWURA Kupandisha Bei Ya Nishati Ya Mafuta Wamiliki Na Madereva Wa Vyombo Vya Moto Mkoani Njombe Wameelezea Athali Zinazoweza Kujitokeza Kutokana Na Mabadiliko Hayo.

Wakizungumza Kwa Nyakati Tofauti Na Waandishi Wa Habari  Baadhi Ya Wamiliki Na Madereva Wa Vyombo Vya Moto Mjini Njombe Wamesema Kuwa Ongezeko Hilo Litakuwa Na Athali Kubwa Kwa Mwananchi Wenye Kipato Kidogo.

Aidha Wamilikili Hao Wameshauri Serikali Kuwashirikisha Wadau Mbalimbali Kabla Ya Kufanya Maamuzi Yanayoweza Kuathili Maisha Ya Wananchi Ikiwemo Ya Upandishaji Wa Bei Za Nishati Ya Mafuta.

Kwa Upande Wao Wamiliki Wa Vituo Vya Mafuta Ya Petrol Na Disel Mjini Njombe Akiwemo Mexon Sanga Wamesema Kuwa Kitendo Cha Serikali Kupandisha Bei Ya Nishati Ya Mafuta Inaathali Kubwa Kwa Wananchi Na Siyo Kwa Wamiliki Wa Vituo Vya Nishati Ya Mafuta.

Akizungumza Na Uplands Fm  Ofisini Kwake Mjini Njombe  Mwenyekiti Wa Wasafirishaji Mkoa  Bwana Donatus Mwamanga Maarufu Kwa Jina La Dosmeza  Amewaomba Wananchi Kuwa Na Subira Kutokana Na Kupanda Kwa Kiwango Kikubwa Cha Nishati Ya Mafuta Ili Kutoa Nafasi Kwa Serikali Kutafakali Juu Ya Bidhaa Nyingine Mbadala Ambayo Itawezesha Unafuu Wa Gharama Za Maisha Ya Wananchi.


No comments:

Post a Comment