Timu ya Taifa ya Tanzania
(Taifa Stars) inayodhamini na kampuni ya bia ya Kilimanjaro, leo imeanza
mazoezi katika uwanja wa Addis Ababa zamani ukifahamka kama (Haille
Sellsie) uliopo jijini Addis Ababa kujiandaa na mchezo dhidi ya Misri
utakaopigwa Juni 14, jijini Alexandria.
Stars ambayo iliwasili jana jioni
jijini Addis Ababa imefikia katika hoteli ya Debre Damo iliyopo eneo na
22 Mazoiria ambapo itakaa kambi kwa kipindi cha wiki moja kujiandaa na
mchezo dhidi ya Mapaharao.
Kocha Mkuu wa timu ya Taifa Stars
Mart Nooij amesema anashukuru vijana wake wamefika salama, na wapo
katika hali nzuri, anaamini wiki moja ya maandalizi nchini Ethiopia
itasaidia kikosi chake kuwa fiti ajili ya mchezo.
Akiongelea kuhusu kambi, kocha
Nooij amesema kwa kuwa mji wa Addis Ababa upo katika ukanda wa juu( mita
2000 kutoka usawa wa bahari), kambi ya mazoezi itakua nzuri kutokana na
wachezaji kufanya mazoezi katika hali hiyo na kwenda kucheza katika
ukanda wa kawaida.
Kuhusu hali ya hewa ni nzuri kwani
baridi iliyopo kwa sasa Addis Ababa ni ya kawaida, hivyo haitaweza
kuwasumbua wachezaji katika maandalizi ya mchezo dhidi ya Misri.
Mchezo kati ya Misri na Tanzania unatarajiwa kuchezwa katika jiji la Alexandria ambalo lipo eneo la bahari ya Mediteranian.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
No comments:
Post a Comment