Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Tuesday, January 27, 2015

ASKOFU WA KKKT DAYOSISI YA KUSINI ISSAYA JAPHET MENGELE AMESEMA ENDAPO KATIBA INAYOPENDEKEZWA HAITAWAFIKIA WANANCHI HADI TAREHE 30 APRIL WATAAMBIA WANANCHI WAIKATAE KWA KUWA HAWAJUI WATAKACHOKIPIGIA

















 AFISA TARAFA YA NJOMBE MJINI LILIAN NYEMELE AKIZUNGUMZIA KATIBA INAYOPENDEKEZWA ITAKAVYOWAFIKIA WANANCHI



 ASKOFU MENGELE AKISISITIZA JUU YA KATIBA INAYOPENDEKEZWA  KWAMBA WATAUNGANA NA MAASKOFU WOTE KOTE NCHINI KUWAAMBIA WANANCHI WAIKATAE KATIBA INAYOPENDEKEZWA KUIPIGIA











Askofu Wa Kanisa La KKKT Dayosisi Ya Kusini  Mkoani Njombe Issaya Japhet Mengele Amesema Endapo Serikali Haitafikisha Katiba Inayopendekezwa Kwa Wananchi Mapema Maaskofu Na  Viongozi Wa Dini Wote Wataungana Nchi Nzima Kuwambia Wananchi Waikataye Katiba Hiyo Kwa Kuwa Hawajui Watakachokipigia Ifikapo April 30 Mwaka Huu.

Askofu Mengele Ametoa Kauli Hiyo Wakati Wa  Zoezi La Uzinduzi Wa Shule Ya Sekondari Ya OSP Ruhuji Ambayo Imeanza Kusimamiwa Na  KKKT Dayosisi Ya Kusini Kupitia  Uongozi Wa Kidugala Seminari Tangu Januari  Mwaka Huu.

Askofu Mengele Amesema Kuwa  Viongozi Wa Dini  Tanzania Walikutana Kwenye Mkutano  Wa Maaskofu Na Viongozi Wengine Wa Dini Wakatoa Mapendekezo Yao Kwa Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa  Tanzania  Kwamba  Kutokana Na Muda Kuwa Mchache  Zoezi La Katiba  Lifanyike Baada Ya Zoezi La Uchaguzi Lakini Wanashangaa Kuona Bado Kauli  Yao Kupuuzwa.

Amesema Kuwa Uchaguzi  Mkuu Wa Mwaka Huu  Maaskofu Walipendekeza Serikali Iepuke Kutumia Siku Za Ibada  Kuweka Siku Ya Uchaguzi  Ambapo Itatakiwa Kuwekwa Siku Ya  Jumatano Na Alhamisi  Ama Juma La Kwanza La Mwezi Wa Kumi.

Afisa Tarafa Ya Njombe Mjini Bi.Lilian Nyemele Akizungumza Mbele Ya Waumini Wa KKKT Dayosisi Ya Kusini Amesema Serikali Inaendelea Na Zoezi La Kuhakikisha Wananchi Wanaipata Katiba Inayopendekezwa Kwa Muda Mwafaka  Huku Akiwataka Wananchi Kutunza Amani Ya Nchi Iliyopo.

Mkuu Wa Shule Ya Sekondari  OSP Ruhuji Bwana ...Akisoma Taarifa Ya Shule Hiyo Amesema Kuwa Pamoja Na Kuwepo Kwa Changamoto Za Ukosefu Wa Mabweni  Na Nyumba Za Walimu Lakini Wanatarajia Kuanza Kuzitatua Changamoto Hizo Na Kuweza Kutoa Elimu Bora Kwa Wanafunzi Ambao Wanakwenda Kujiunga Shuleni Hapo.


Tulimtafuta Mkuu Wa Wilaya Ya Njombe Bi.Sarah Dumba  Ili Aweze Kuzungumzia Katiba Inayopendekezwa  Kama Itawafikia Lini Wananchi  Na Yeye Akawa Na Haya Kama Anavyotueleza Hapa

No comments:

Post a Comment