Tuesday, November 4, 2014
MKUU WA WILAYA YA NJOMBE AWA HIMIZA MADIWANI KUANZA UJENZI WA MAABARA TATU NOVEMBA 30 WAWE WAMEKAMILISHA
HAWA NI MADIWANI WA HALMASHAURI YA MJI WA NJOMBE WAKIWA KWENYE KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI
MKUU WA WILAYA YA NJOMBE BI.SARAH DUMBA AKIZUNGUMZA NA MADIWANI WA HALMASHAURI YA MJI WA NJOMBE
Halmashauri ya Mji wa Njombe Imeshindwa Kufikia Lengo la Kukusanya mapato kwa asilimia 25 Ambapo Pamoja na Mambo Mengine Hali hiyo imedaiwa kuchangiwa na Baadhi ya Watendaji wa Vijiji na Mitaa Kutokusanya kama Ilivyokusudiwa Kwenye Vikao vya Baraza la Madiwani lililopita.
Kauli hiyo Imetolewa na Mwenyekiti Wa Baraza la Madiwani Wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Edwin Mwanzinga Wakati akifungua Kikao cha Baraza Hilo Ambapo Amewataka Madiwani kusimamia Kwa makini utekelezaji na Ukusanyaji wa Mapato Kwa kushilikiana na W atendaji Kubuni Mbinu za kukusanya mapato Kama ilivyopitishwa kwenye bajeti ya Mwaka wa fedha 2014/2015.
Aidha Bwana Mwanzinga amesema kuwa Halmashauri imefikia kiwango cha asilimia 15 za Ukusanyaji wa Mapato Ikiwa Katika Bajeti ya Mwaka wa Fedha Ya 2014/2015 imejipangia kukusanya Zaidi ya shilingi Bilioni mbili na milioni mia Mbili themanini Ikiwa ni mapato ya ndani Ambapo elimu inatakiwa kutolewa kwa walipa kodi ili kutekeleza Maazimio yake Huku agenga ya Ujenzi wa vibanda nayo ikizungumziwa.
Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi. Sarah Dumba akitoa Salamu za Serikali Amesema kuwa Agenda Kubwa kwa wakati huu ni kujenga Maabara Tatu Ambapo amewasisitiza Madiwani kuhakikisha wanafanikisha jukumu hilo kwa Kushirikiana na wananchi Kuchangia ujenzi huo huku Akiwapongeza Wananchi wa Kata za Makowo na Matola kwa kukamilisha ujenzi huo Ambao ni Agizo la Profesa Rais Kikwete.
Bi. Dumba amesema Mkurugenzi anatakiwa kulipatia kipa umbele Agizo hilo la Ujenzi wa Maabara Tatu Ambapo pamoja na Mambo Mengine ametaka wananchi na viongozi wa Vijiji na kata kusimamia hifadhi ya mazingira kwa kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wahusika wanaoharibu mazingira hayo na kuacha kulima kwenye vyanzo vya maji.
Wakichangia Mada zilizowasilishwa kwenye Baraza hilo Madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Wamehoji kupandishwa kwa kodi ya ushuru wa biashara ndogondogo kuanzia shilingi mia mbili hadi shilingi mia tano,kujengwa kwa vibanda katika Soko Kuu la Njombe Mjini na La Wakulima na kutaka kutengwa kwa bajeti ya kutosha kwaajili ya Miundombinu ya barabara.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment