JESHI LA WANANCHI WA TANZANIA JWTZ WAKIINGIA MAKAMBURINI KUTOA HESHIMA ZA MWISHO
MWENYE NGUO NYEUPE NA KITAMBAA CHEUPE KICHWANI NI MKE NA MAREHEMU
MWENYEKITI WA MTAA WA IDUNDILANGA AUGUSTINO MGEN AKIWA KWENYE MAKABURI YA MPECHI AKITOA NASAHA CHACHE
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Captain Mstaafu Asseri Msangi Amewataka Watanzania Kuendelea Kudumisha Amani ya Nchi Ili Kulinda Umoja na Mshikamano Kwa Watanzania.
Kauli Hiyo Imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi.Sarah Dumba Kwa Niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe Alipoongoza Mazishi ya Meja Jenerali Mstaafu Aidan Mfuse Aliyefariki Oktoba 29 Mwaka Huu Nchini India Alikokuwa Anapatiwa Matibabu.
Bi.Dumba Amesema Kuwa Heshima za Mwisho za Meja Jenerali Mstaafu Mfuse Mkoani Njombe Zimewadhihilishia Watanzania na Wakazi wa Njombe Kuwa Taifa Bado Lina Ulinzi Mkubwa na Hivyo Kila Mmoja Anawajibu wa Kulinda na Kutunza Amani ya Taifa la Tanzania.
Historia Fupi ya Marehemu Meja Jenerali Aidan Mfuse Iliyosomwa na Mwakilishi wa Jeshi la Wananchi Meja Jenerali Chacha Imeeleza Kuwa Marehemu Mfuse Amelitumikia Taifa la Tanzania Kwa Miaka 37 Kwa Kushika Nyadhifa Mbalimbali Pamoja na Kuongoza Vikosi,Vyuo Mbalimbali Vya Mafunzo ya Jeshi Nje na Ndani ya Nchi Hadi Alipostaafu Kwa Lazima Mwaka 2005.
Amesema Hadi Kifo Kinamkuta Akiwa Nchini India Kwa Matibabu Amekufa Akiwa na Cheo Cha Meja Jenerali Ambapo Ametunukiwa Nishani Mbalimbali na Amiri Jeshi Mkuu Ikiwa ni Pamoja na Kutunukiwa Nishani ya Uongozi Uliotukuka.
Mazishi ya Meneja Jenerali Aidan Mfuse Yamefanyika Katika Makaburi ya Mpechi Mjini Njombe Baada ya Mwili wa Marehemu Kuwasili Hapo Jana Toka Jijini Dar es Salaam Ambako Mwili Ulifikia Toka Nchini India Alikokuwa Anasumbuliwa na Maradhi ya Moyo.
Bwana Alitoa na Bwana Ametwaa Jina la Mungu Lihimidiwe.
No comments:
Post a Comment