Na Michael Ngilangwa
Jeshi la Polisi Mkoani Njombe Linawashikilia Watu watatu Kwa tuhuma za kusababisha
vifo vya Watu Watatu vilivyotokea Kwa Nyakati za Matukio Tofauti Yakiwemo Matukio
Mawili ya Ajali yaliotokea kata ya Ramadhani Katika Mitaa ya Wikichi na Ramadhani
Mjini Njombe.
Katika Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe SACP Fulgence
Ngonyani imebainisha Kuwa Mtaa wa Ramadhani yametokea matukio Matatu ya Ajali ya
magari Ambazo zimesababisha vifo vya watu wa wili na Majeruhi Mmoja wa Mtaa wa
Kibena matukio yaliotokea jana kwa nyakati tofauti.
Taarifa hiyo ya Jeshi la Polisi iliyosainiwa na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe
SACP Fulgence Ngonyani imebainisha kuwa ajali ya kwanza kwanza Mwanafunzi wa
shule ya msingi Ramadhani mwenye miaka 9 Hamphrey Mwangisa amefariki dunia kwa
kugongwa na gari namba T846 BCL aina ya Toyota mali ya Sament Sanga lililokuwa
likiendeshwa na Nehemia Eskata Sanga mkazi wa Makambako.
Aidha tukio la pili mkazi wa Mfereke James Mpete Ambaye alikuwa akiendehsa pikipiki
T225CUQ T BETTER amefariki dunia baada ya kugongwa na gari lenye Namba T 236
BOH Toyota Land Cruzer Ikiendeshwa na Bora Izack Kamwele mkazi wa Katavi ili
mgonga mwendesha pikipiki huyo akiwa maeneo ya Mtaa wa Wikichi kata ya Ramadhani
na kufariki dunia papo hapo Tukio lililotokea novemba 3 majira ya saa 11 jioni.
Taarifa hiyo imesema kuwa tukio la Tatu mtoto mwenye umri wa miaka 2 Francis
Mangula amefariki dunia kwa kulaliwa na mama yake Roswita Sanga wakati akitokea
kilabuni ambaye amedaiwa kulewa pombe tukio lililotokea jana novemba tatu majira ya
saa kumi na mbili jioni katika kijiji cha Itunduma kata ya Mtwango.
Katika Tukio lingine gari lisilofahamika namba zake na wala mmiliki wa gari hilo
limemgonga Mtembea kwa Miguu Debasis Majumdah mwenye bumri wa miaka 49
muhindi Ambaye ni mfanyakazi wa kampuni ya Tanwat na kusababisha majereha ya
kuvunjika mikono na miguu katika tukio lililotokea jana majira ya saa moja jioni.
Kufuatia kutokea kwa matukio hayo Jeshi la polisi Mkoa wa Njombe linawashikilia Watu
watatu wakiwemo madereva wawili waliosababisha vifo hivyo na Mama mmoja mkazi wa
Itunduma Kata ya Mtwango huku likiendelea kumtafuta mmiliki na dereva wa gari
lililosababisha ajali na kukimbilia kusiko julikana na kwamba uchunguzi utakapo kamilika
washtakiwa watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.
No comments:
Post a Comment