Mara Baada ya Ibada katika Kanisa la Azania Front wakati wa kuadhimisha miaka 85 ya kuzaliwa ya aliyekuwa Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Philemoni Mgaya
Baadhi ya waumini mbalimbali wakiwa nje baada ya Ibada
Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Mstaafu Philemoni Mgaya akiwa katika siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake
Keki
Waziri Mkuu
Mstaafu Cleopa Msuya akimpongeza aliyekuwa IGP Philemoni Mgaya
Mzee Timothy Msangi akieleza Historia fupi ya IGP Mstaafu Philemoni Msangi
Askofu Mkuu
wa Kanisa la Kilutheli Tanzania (KKKT) Alex Malasusa akitoa salam za Pongezi kwa IGP mstaafu
Mshauri
wa kimataifa wa Kujitegemea wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Limited
James Rugemalira akitoa pongezi zake kwa IGP Mstaafu na kuelezea Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Limited
Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni hiyo Benedicta Rugemalira akitoa salam za Pongezi kwa IGP mstaafu
Waziri wa Habari na Utangazaji Fenera Mukangara akimpa mkono wa Pongezi IGP mstaafu
Wakiwa katika Furaha
Huduma ikiendelea huku waalikwa wakiwa wanafurahia na kupata vinywaji kutoka kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirit Limited Kinywaji cha Windhoek Larger na Windhoek Draught
Watu mbalimbali wakiwa katika Sherehe hiyo
Burudani ya nguvu
WAZIRI Mkuu
Mstaafu Cleopa Msuya amewaomba watanzania
kuwa na tabia ya utii wa sheria, uaminifu na uadilifu katika nafasi zao
wanazozitumukia katika Taifa la Tanzania.
Msuya
aliyasema hayo katika sherehe ye kuadhimisha miaka 85 ya kuzaliwa ya aliyekuwa Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Philemoni Mgaya iliyofanyika katika Hotel ya
Protea , Court Yard jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu
Mstaafu alieleza kuwa tabia aliyoionyesha Mgaya wakati wa utumishi wake
serikalini inapaswa kuigwa na watanzania wote.
“Huyu ndiye
Mtanzania halisi aliyelelewa vizuri kuitumikia nchi yake. Hana makuu, ni mkweli
na mwadilifu. Akiahidi kufanya jambo fulani analitekeleza bila kuchelewa.
Tunahitaji uwajibikaji wa namna hii,” Msuya alisisitiza.
Alisema kuwa
Mgaya alikuwa kiongozi hodari ambaye alisimamia vyema kiapo na kazi zake na
kipindi chake cha uongozi alikuwa akitoa
amri zinatekelezwa mara moja.
Naye Mshauri
wa kimataifa wa Kujitegemea wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Limited
James Rugemalira alitoa wito kwa watanzania kuendele kuunga mkono jitihada za kuendeleza maeneo mbalimbali ya
kiuchumi ikiwemo viwanda.
Aliwasihi wadau
kutoa ushirikiano kwa kampuni yake inayosambaza
bia aina ya Windhoek Larger na Windhoek Draught ambayo inadhamira ya kujenga
kiwanda cha kuzalisha bia hizo hapa nchini.
“Tunatafuta
maeneo Kilimanjaro, Tanga na Bukoba ili tuweze kujenga kiwanda hapa nchini.
Tumedhamilia kufanya hivyo na tutafanya,” Rugemalira alisisitiza.
Naye Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni hiyo Benedicta Rugemalira aliwashukuru wananchi kwa
kukubali kujumuika pamoja katika hafla hiyo na kumwomba Mzee Mgaya aendelee kuwapa
mwongozo wa namna ya kuenenda katika maisha.
Askofu Mkuu
wa Kanisa la Kilutheli Tanzania (KKKT) Alex Malasusa aliwaomba watanzania kuwa na
moyo wa unyenyekevu na kujitolea kulitumikia taifa katika utumishi wao kama ilivyokuwa
kwa IGP mstaaafu Mzee Mgaya.
Wageni wengine
waliohudhuria hafla hiyo ni Waziri wa Habari na Utangazaji Fenera Mukangara, Katibu
Mkuu Msaaafu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Balozi Bakari Mwapachu, Balozi Antoni
Nyaki na wazee wengine maarufu kama Timothy Msangi.
No comments:
Post a Comment