Thursday, November 6, 2014
ASKOFU WA KANISA LA KKKKT DIOSISI YA KUSINI ISSAYA JAPHET MENGELE AFUNGUA KITUO CHA KULELEA WAZEE MTAA WA KIBENA MJINI NJOMBE
ASKOFU WA KANISA LA KIINJILI LA KIKRISTO LA KILUTHEL TANZANIA DIOSISI YA KUSINI ISSAYA JAGPET MENGELE AKIWA NDANI BAADA YA KUFUNGUA JENGO LA KITUO CHA KULELEA WAZEE KATIKA MTAA WA KIBENA
ASKOFU MENGELE AKIFUNGUA KITUO CHA KULELEA WAZEE KILICHOPO MTAA WA KIBENA.
HAWA NI WAFADHILI TOKA MAREKANI AMBAO NI WAFADHILI WA WASHARIKA WA CENTRE LUTHELAN ELK LIVER MINESOTA U.S.A WAKIWASILISHA TAARIFA ZAO
MCHUNGAJI WA KANISA LA KIINJILI LA KIKRISTO LA KILUTHEL TANZANIA USHARIKA WA KIBENA MCHUNGAJI NELSON KADUMA AKISOMA TAARIFA YA UJENZI KWA ASKOFU WA DAYOSISI YA KUSINI ISSAYA JAPHET MENGELE.
HAWA NI BAADHI TU YA WAZEE WALIOWAKILISHA WAZEE WENZAO
ASKOFU MENGELE AKIFUNGUA KITUO HICHO BAADA YA KUKATA UTEPE
PICHA NA KAYOMBO STATIONARY
Askofu Wa Kanisa La Kiinjili La Kilutheli Tanzania Diosisi Ya Kusini Japhet Mengele
Amefungua Jengo La Kutuo Cha Kulelea Na Kutoa Huduma Kwa Wazee Kilichopo Mtaa
Wa Kibena Ambacho Kimejengwa Kwa Ushirikiano Wa Usharika Wa Kibena Na
Matiganjora Lililogharimu Dola Elfu 89.5 Za Kimalekani Sawa Na Zaidi Ya Shilingi Shilingi Milioni 80 Za Kitanzania .
Akizungumza Wakati Wa Kufungua Kituo Hicho Cha Kulelea Wazee Askofu Wa Kanisa La Kiinjili La Kikristo La Kiluthel Tanzania Issaya Japhet Mengele Amepongeza Kwa Mawazo Ya Kujenga Kituo Hicho Ambacho Kitawasaidia Kwa Kiasi Kikubwa Wazee Ambapo Ni Wajibu Kwa Kila Mkristo Na Jamii Kwa Ujumla Kuhakikisha Wazee Hao Wanapata Mahitaji Mbalimbali Ikiwemo Huduma Za Afya.
Aidha Askofu Mengele Amewaondoa Hofu Wazee Wote Watakao Kwenda Kwenye Kituo
Hicho Kupata Huduma Za Matibabu Na Kwamba Diosisi Hiyo Imejipanga Kikamilifu Kuhakikisha Wazee Hao Wanapata Matibabu Yaliosahihi Na Huduma Nyingine Muhimu Ambapo Amesema Ataendelea Kuwapeleka Viongozi Wa Dini Na Serikali Ili Kushuhudia Kituo Hicho Kinavyofanya kazi.
Akizungumza Mara Baada Ya Kufunguliwa Kwa Kituo Cha Kuwalelea Wazee Kilichopo
Mtaa Wa Kibena Mchungaji Wa Kanisa La Kiinjili La Kikristo La Kilutheli Tanzania Usharika Wa Kibena Mch. Nelson Kaduma Amesema Kuwa Kuanzishwa kwa Kituo Hicho Kutasaidia kuwakomboa wazee wengi Mkoani Njombe Na Watanzania Wote Ambapo Kimejengwa Kwa Ufadhili wa washarika wa Centre Luthelan Elk Liver Minesota U.S.A.
Aidha Mchungaji Kaduma Amesema Kituo Hicho Cha Kulelea Wazee
Kimefikia Hatua Za Mwisho Kukamilika Na Kwamba imebakia Kuweka Samani Za Ndani na mahitaji mengine madogomadogo ya ndani.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment