Sunday, September 14, 2014
WAZAZI WALIODAIWA KUTELEKEZA MTOTO WAO WAPATIKANA
AFISA USTAWI WA JAMII WA HALMASHAURI YA MJI WA NJOMBE HOSEA YUSTO BAADA YA KUWAPATA WAZAZI HAO ANAZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI AKIWA OFISINI KWAKE.
HAWA NI WAZAZI WA MTOTO HAMIDA SANGA ALIYEDAIWA KUTELEKEZWA NA WAZAZI WAKE KWA MUDA MREFU NA KUPELEKEA KUPATIWA MISAADA NA SHULE YA MSINGI LUHUJI
HIZI NI OFISI ZA HALMASHAURI YA MJI WA NJOMBE ZA IDARA YA KILIMO,MAENDELEO NA USTAWI WA JAMII
Hatimaye wazazi wa mtoto Hamida Sanga mkazi wa Mtaa wa Kwivaha wamejitokeza na kukanusha kauli za viongozi wa serikali wa kata,taarafa,shule na mtaa huo ya kwamba wametelekeza mtoto wao tangu mwezi april mwaka huu huku wakikili kwenda kuuguza mgonjwa katika hospitali ya Ikonda kwa siku chache na kuwepo kwa uzembe wa kutokuwa karibu na walimu shuleni.
Hatua ya Wazazi hao kutolea ufafanuzi huo imefuatia kituo hiki kurusha taarifa za kudaiwa kutelekezwa kwa watoto hao na wazazi wao na kusaidiwa mahitaji na shule ya msingi Luhuji jambo ambalo lilimlazimu diwani wa kata na afisa taarafa ya Njombe mjini Angela Mwangeni na Lilian Nyemele kuagiza uongozi wa mtaa huo kuwatafuta wazazi hao popote watakapo patikana na kuchukuliwa hatua za kisheria.
Aidha wazazi hao wamesema kuwa walikuwa na mawasiliano na mtoto huyo pindi wakiwa hospitali ya Ikonda na kwamba walitoa namba kwa mwalimu wa ambaye anafundisha shuleni hapo na kwamba mtoto huyo alidanganya walimu kwamba ametelekezwa lakini wazazi bado wapo naye.
Afisa ustawi wa jamii wa halmashauri ya mji wa Njombe bwana Hosea Yusto amesema mtoto huyo imeonesha alikuwa anaishi na mzazi wake ambaye ni baba yake ,mama yake akiwa Makete lakini kutokana na uzembe uliojitokeza kwa wazazi hao na tatizo la kukwepa kwenda shuleni kupeleka michango imepelekea mtoto kuonekane ametelekezwa.
Bwana Yusto amesema wakati mama wa mtoto akiwa Wilaya ya Makate kwa matibabu, mtoto alikuwa na baba yake nyumbani Na kwamba baba huyo anafanya kazi ya kupasua mbao msituni Jambo ambalo limesababisha baba huyo wakati mwingine kushindwa kurudi licha ya kudaiwa huduma zilikuwa zikitolewa kwa mtoto.
Kwa upande wake diwani wa viti maalumu wa kata ya Njombe mjini bi.Angela Mwangeni amesema jitihada za kutembelea shule nyingine za msingi katika kata hiyo bado zinaendelea ili kubaini baadhi ya wazazi wanaowaacha watoto bila kutoa huduma kwa watoto.
Mwenyekiti wa kamati ya shule ya msingi Luhuji bwana Norasco Kilasi amesema utetezi wa wazazi wa mtoto huo kuhusiana na Suala hilo na kwamba wazazi hao walitelekeza kwa kukwepa majukumu ya kuwalea watoto. na utetezi wao umedaiwa siyo wa kweli.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment