Library ikiwa na vitabu vya kutosha
.Msimamizi
wa Library katika shule ya Southern Highlands Mafinga Glory Mgullah
kulia akimwekekeza mgeni rasmi katika mahafali ya 14 ya darasa la
saba shuleni hapo Bw Nasibu Mengele (wa pili kushoto) vitabu mbali
mbali vilivyomo katika Library ya shule hiyo wa kwanza kushoto ni
mkuu wa shule hiyo Bi Mary Mungai na wa tatu kushoto mkuu wa shule hiyo
Jason Nyang'ware
katibu mwenezi wa CCM Mufindi Daudi Yassin akiwa na mjukuuu wake ambae ni mhitimu wa darasa la saba Southern Highlands Mafinga leo |
Yassin akiwa na mjukuu wake narafiki wa mjukuu huyo |
UONGOZI
wa shule ya Southern Highlands Mafinga mkoani Iringa umesema kuwa
toka shule hiyo ilipoanzishwa zaidi ya miaka 13 sasa haijapata
kufelisha mwanafunzi hata mmoja na kuwataka wazazi wa wanafunzi 48
waliohitimu darasa la saba mwaka huu kujiandaa kuwapeleka watoto wao
wote sekondari zenye sifa .
Mkurugenzi
mtendaji wa shule hiyo Bi Mary Mungai juzi wakati wa mahafali ya
14 ya darasa la saba katika shule hiyo na kuwa ubora wa
elimu ambao umeendelea kutolewa shuleni hapo ndio sababu ya
wazazi kuchagua shule hiyo kwa ajili ya kuwapatia elimu bora
watoto wao na si bora elimu.
"Kwa
mwaka huu haya ni mahafali ya 14 na wanafunzi wote ni 48 ndio
walifanya mtihani wa Taifa wa darasa la saba wakiwemo wasichana 24 na
wavulana 24 hivyo kutokana na uwezo wa wanafunzi hawa katika mitihani
yao mbali mbali shule inategemea kufaulisha tena wanafunzi wote
.....hakuna hata mmoja atakayefeli "
Kwani
alisema katika rekodi ya shule hiyo toka ilipoanzishwa kama
shule ya Msingi hakuna hata mwaka mmoja ambao mwanafunzi alishindwa
kuchaguliwa kujiunga na elimu ya sekondari nchini.
Alisema
kuwa shule ilianzishwa mwaka 1994 kama chekechea kwa jina la
Lusungu Day Care Center ,Mwaka 1997 ilikuwa na kuanza shule ya
msingi -primary school ndiyo sasa inaitwa southern Highlands yenye
usajili wake namba IR03/7/001 ya mwaka 1997 ambapo imekuwa ni
shule ya pili kufunguliwa baada ya Brook Bond
“
Uongozi wa shule umekuwa ukihakikisha unakuwa na mpango endelevu
wa kuboresha mazingira ya shule pamoja na kuboresha elimu zaidi
ili shule hiyo kuendelea kubaki ya mfano katika taalum mkoa wa
Iringa na nje ya mkoa wa Iringa
Alisema
mbalia ya wanafunzi wa shule hiyo kuwa na utaratibu wa kufundishwa
masomo mbali mbali darasani ila bado shule imekuwa na utaratibu wa
kuwapeleka wanafunzi katika mafunzo maeneo mbali mbali yakiwemo ya
vivutio vya utalii katika Tanzania bara na visiwani lengo likiwa ni
kukuza uelewa zaidi wa watoto hao.
Bi
Mungai alisema kuwa mbali ya kutembelea maeneo mbali mbali ya nje
ya mkoa pia shule imekuwa na utaratibu wa kuwapeleka kujifunza
pia katika mashirika yaliyomo ndani ya mkoa wa Iringa na Njombe .
Hata
hivyo alisema ushirikiano mzuri ambao wazazi wamekuwa
wakionyesha katika shule hiyo hivi sasa wapo katika mkakati wa
kuanzisha shule ya sekondari kati ya mwaka 2020-2025 na kuwa japo
inawezekana kuanza shule ya sekondari kati ya mwaka 20215 kutokana na
mipango mizuri iliyopo .
Kwa upande wake kaimu afisa elimu wa Nasibu A. Mengele
alisema kuwa kati ya shule ambazo zimekuwa zikiupatia sifa mkoa
wa Iringa kwa kufanya vizuri katika mitihani ya darasa la saba ni
pamoja na shule hiyo ya Southern Highlands Mafinga hivyo wao kama
viongozi wa elimu wataendelea kuitolea mfano shule hiyo kila sehemu
na ikiwezekano kuitangaza zaidi ili wazazi kusomesha watoto wao
katika shule hiyo.
Mengele
ambae alikuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo alisema kuwa
uwekezaji mzuri uliofanywa na Bi Mungai katika shule hiyo ni mfano
pia wa kuigwa kwa wana taaluma wengine kuangalia uwezekano wa
kuwekeza katika elimu kama alivyofanya mkurugenzi wa shule hiyo baada
ya kustaafu nafasi yake ya uafisa elimu wilaya aliamua kuwekeza
katika elimu na hata kuufanya mkoa wa Iringa kusifika kutoka ana
shule hiyo kuwa ya mfano katika ufaulu .
Wakati huo huo uongozi wa shule
hiyo umetumia sherehe hizo kuwatangazia wazazi nafasi za masomo na
kuwa nafasi kwa wazazi wote nchini wanaotaka watoto wao kupata elimu
katika shule hiyo zipo na kuwa hawana mipaka kwa wanafunzi kutoka
ndani na nje ya nchi wanapokelewa .
Hivyo alisema nafasi zipo kwa Shule ya
msingi ya English medium, Southern Highlands School, kwa watoto wa
chekechea, darasa la kwanza mpaka darasa la tatu (nursery, na class 1-3)
na watoto wa darasa la tano (5) na la sita (6).
Alisisitiza kuwa iwapo mzazi kote
nchini na nje ya nchi anahitaji kuleta mtoto wake basi kuweza
kuwasiliana kupitia njia zifuatazo:
Simu:
026-2772661
0752-840884
0756-749151
Email:
Southernhighlands97@hotmail.com
No comments:
Post a Comment