Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Monday, November 18, 2013

WATU WAWILI WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOANI NJOMBE KWA TUHUMA ZA MAUAJI HUKU KIBAKA MMOJA AKIPEWA ONYA NA BAADHI YA WANANCHI MJINI NJOMBE

 HAPA HUYU BWANA ANADAIWA KUHUSIKA NA UTAPELI  MAENEO YA CCM MJINI NJOMBE LEO AMEKAMATWA AKIWA PEKE YAKE LAKINI MWENZAKE AKAKIMBIA BAADA YA KUONA MWENZAKE KAKAMATWA

 HAPA NI BAADA YA KUACHIWA AJIELEZE MBELE YA WANANCHI WA NJOMBE MJINI
 HUYU NI KIJANA ANAYEDAIWA KUHUSIKA KUWAUZIA WANANCHI VICHUPA KWA KUWADANGANYA KWAMBA NI MADINI PAMOJA NA UTAPELI WA FEDHA KWA WANANCHI NA HAPA WANANCHI WAMEMKAMATA NA KUANZA KUMUHOJI



AKITOA MATUKIO YALIOJIRI KWA MASAA 24 YALIOPITA.

Jeshi la Polisi Mkoani Njombe Limethibitisa Kutokea Kwa Matukio Matatu ya

Mauwaji Huku Likiwashikilia Watu Wawili Kwa Tuhuma za Kuhusika na Mauwaji

Hayo Likiwemo la Dereva Pikipiki Enock Kihindo Aliyeuwawa Kwa Kunyongwa na

Kisha Mwili Wake Kutupwa Porini.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe ACP Fulgency Ngonyani Amesema Mnamo

Novemba 16 Mwaka Huu Marehemu Enock Kihindo Alikutwa Akiwa Amefariki Huki

Mwili Wake Ukiwa Umetupwa Porini Barabara ya Kuelekea Yakobi.

Marehemu Enock Kihindo Aliondoka Katika Kituo Chake cha Kazi Novemba Kumi

Mwaka Huu Majira ya Jioni Baada ya Kukodiwa na Mtu Ambaye Alidai Ampeleke

Maeneo ya Yakobi na Kwamba Katika Tukio Hilo Jeshi la Polisi Linamshikilia Mtu

Mmoja Ambaye Jina Lake Limehifadhiwa Kwa Mahojiano Zaidi.

ACP Ngonyani Amesema Tukio la Tatu Limetokea Katika Kijiji cha Mavala Wilayani 

Ludewa Ambapo Charles Luoga Mwenye Umri wa Miaka 87 Amefariki Baada ya

Kuungua Kwa Ajali ya Moto Huku Taarifa Zikieleza Kuwa Marehemu Alikuwa

Anaishi Pekee Yake Shambani  Hali Iliyopelekea Kushindwa Kujiokoa Baada ya Ajali

Hiyo ya Moto Kutokea.

Kamanda Huyo wa Polisi Mkoa wa Njombe Amesema Jeshi Hilo Linaendelae na

Uchunguzi wa Vyanzo Vya Matukio Hayo na Pindi Utakapo Kamilika Wahusika

Watafikishwa Mahakamani Kujibu Tuhuma Zinazowakabili Huku ACP Ngonyani

Akiwataka Wananchi Kutojichukulia Sheria Mkononi.

No comments:

Post a Comment