Wednesday, November 20, 2013
SIKU CHACHE BAADA YA DEREVA BODABODA KUUWAWA NA WATU WASIYOFAHAMIKA,JESHI LA POLISI LEO LIMEWAKUTANISHA WAMILIKI NA MADEREVA BODABODA NA KUWATAKA KUIMARISHA URINZI SHIRIKISHI ILI KUKABILIANA NA UHARIFU
BODABODA ZIKIWA ZIMEPAKIWA WAKATI WAMILIKI WAKE WAKIWA NDANI YA UKUMBI WA POLISI NJOMBE LEO
WAMILIKI NA MADEREVA BODABODA WAKIINGIA NDANI YA UKUMBI WA POLISI NJOMBE KWENYE KIKAO NA POLISI KILICHO LENGA KUJADILIA SUALA LA KUPUNGUZA AJALI NA MATUKIO YA UHARIFU WA KUIBIWA PIKIPIKI NA MAUWAJI YANAYOFANYWA NA MAJAMBAZI MKOANI NJOMBE
AFISA USALAMA WA BARABARANI MKOA WA NJOMBE MARO CHACHA AKIWAELEZA MADREVA HAO LENGO LA KUWAITISHA WAMILIKI NA MADEREVA WA BODABODA HIZO
MNADHIMU MWANDAMIZI NA MRAKIBU WA JESHI LA POLISI MKOA WA NJOMBE FOCUS MALENGO AKIZUNGUMZA NA MADEREVA NA WAMILIKI WA BODABODA KATIKA UKUMBI WA JESHI LA POLISI MKOA WA NJOMBE LEO.
AFISA USALAMA WA BARABARANI AKITOLEA UFAFANUZI SABABU ZA JESHI HILO KUCHELEWA KUFIKA KWA WAKATI KWENYE TUKIO PINDI WANAPOPATA TAARIFA KWAMBA NI KUTOKANA NA JESHI LA POLISI KWENDA KWENYE TUKIO LINATAKIWA KUWACHUKUA MADAKTARI KWENDA NAO LAKINI UKIFIKA OFISI ZA MADAKTARI UNAKUTA WATAALAMU WAKO KUWAHUDUMIA WAGONJWA HIVYO INALAZIMU KUSUBIRI NDIPO WAONDOKE NAO JAMBO LINALOPELEKEA KUCHELEWA
KAIMU MWENYEKITI WA BODABODA MJINI NJOMBE BWANA MASUDI KOMBA AKITOA NASAHA KIDOGO KWA MADEREVA WENZAKE
BAADA YA KUMALIZA MAZUNGUMZO KAMANDA WA POLISI NA KIKOSI CHAKE AKITOKA NDANI YA UKUMBI WA POLISI NJOMBE NA KUELEKEA KWENYE MAJUKUMU MENGINE
BODABODA NAO WAKITOKA KUELEKEA KWENYE VITUO VYAO VYA KAZI
Jeshi la Polisi Mkoani Njombe Leo Limekutana na Wamilili na Madereva Pikipiki
Maarufu Kama Bodaboda Mjini Njombe Kwa Lengo la Kujadili Jinsi ya Kukabiliana
na Matukio ya Uhalifu na Vitendo Vya Kutekwa na Kuuwawa Kwa Madereva Pikipiki
Hao.
Katika Kikao Hicho Jeshi la Polisi Limewashauri Wamiliki na Madereva Pikipiki Hao
Kuunda Vikundi Vitakavyokuwa Vikisaidiana na Jeshi Hilo Katika Doria na
Kuwabaini Watu Wanaojihusisha na Vitendo Vya Uhalifu na Matukio ya Mauwaji
Kwa Madereva Hao Pamoja na Kuporwa Pikipiki Zao.
Akiongea Kwenye Kikao Hicho Afisa Mnadhimu wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe
Focus Malengo Amekemea Baadhi ya Tabia ya Madereva Wanaouza
Pikipiki za Waajiri Wao na Kudai Kuwa Wameibiwa na Kuwataka Madereva
Kujijengea Tabia ya Kuwaaga Wenzake Pindi Anapopata Mteja.
Kwa Upande Wake Afisa Usalama Barabarani Mkoani Njombe Maro Chacha
Amewashukuru Baadhi ya Wamiliki na Madereva Pikipiki Hao Kwa Kufuata Sheria
na Matumizi Sahihi ya Barabara , Huku Akisema Bado Kuna Changamo Kwa Baadhi
ya Wamiliki na Madereva Pikipiki Hao Ambao Wanakaidi Sheria za Barabarani
Ikiwemo Mwendokasi Hasa Katika Barabara ya Mtaa wa Kambarage
Awali Wakiuliza Maswali Kwa Kamanda wa Jeshi la Polisi Wamiliki na Madereva
Pikipiki Hao Wametaka Jeshi la Polisi Kuwahi katika maeneo ya Matukio Pindi Wanapopatiwa Taarifa Kuhusiana na Uhalifu ,Huku Mwenyekiti Wao Bwana Masoud Komba Akiahidi Kuyafanyia Kazi Yale Yote Waliyoshauriwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment