Wednesday, November 20, 2013
NJOMBE MJI FC LEO YAGAWA DOZI YA MAGOLI 4-2 DHIDI YA LUPONDE FC KATIKA LIGI YA TAIFA NGAZI YA MKOA KWA MKOA WA NJOMBE
MASHABIKI WAKIENDELEA KUSHUHUDIA KANDANDA UWANJANI KATI YA NJOMBE MJI FC NA LUPONDE FC KATIKA UWANJA WA SABASABA MJINI NJOMBE LEO
WACHEZAJI WA TIMU YA NJOMBE MJI WAKISUBIRIA KUINGIA KUIKABILI LUPONDE FC KATIKA UWANJA WA SABASABA
HAWA NI TIMU YA LUPONDE FC WAKIKABILIANA NA TIMU YA NJOMBE MJI
HII NI TIMU YA NJOMBE MJI WAKIWA UWANJANI KUIKABILI TIMU YA LUPONDE FC
Timu ya mpira wa miguu ya Njombe mji leo imeshuka dimbani kuikabili timu ya Luponde fc katika ligi ya Taifa ngazi ya mkoa ambapo imeweza kuandika magoli manne dhidi ya timu ya Luponde fc ambayo imepata magoli mawili katika mchezo ulichezwa uwanja wa sabasaba mjini Njombe.
Timu ya Njombe mji ilianza kuandika goli la kwanza kupitia mshambuliaji wake Abdalah Zungu kuiandikia timu yake goli la kwanza katika kipindi cha kwanza kwa kuuweka mpira kinywani na kupachika goli la kwanza kunako dakika ya 22 huku Francis Anyagise akiandika magoli mawili katika dakika ya 80 na 84 katika kipindi cha pili.
Wakati mpira ukiendelea uwanjani hapo mshambuliaji wa timu ya Njombe mji Musa Maginga aliweza kuhitimisha dakika tisini kwa kuogeza goli la nne na kutoka na ushindi kwa leo katika uwanja huo.
Wakati huoi timu ya Luponde fc iliweza kujipatia mabao yake kupitia washambuliaji wake Cardo Haule na Gila Mdoe kunako dakika ya 85 na dakika ya 48 katika kipindi cha pili.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment