Tuesday, November 19, 2013
CHAMA CHA USHIRIKA CHA AKIBA NA MIKOPO CHA SACCOS CHA NJOMBE MJINI LEO KIMEFANYA MKUTANO MKUU KATIKA UKUMBI WA TURBO
MWENYEKITI WA CHAMA CHA USHIRIKA CHA AKIBA NA MIKOPO SACCOS YA NJOMBE MJINI ERNEST NYANDOA AKIWA KWENYE MKUTANO HUO
MGENI RASMI AFISA USHIRIKA WA HALMASHAURI YA MJI WA NJOMBE WILLIAM KINYAGA AKITOA HOTUBA YAKE KATIKA UKUMBI WA TURBO NJOMBE MJINI
AFISA MWANDAMIZI WA SHIRIKA LA HIFADHI YA JAMII NSSF MKOA WA NJOMBE BWANA NGUSA SOMOLO AKITOA NASAHA KWA WANACHAMA WA SACCOS YA NJOMBE MJINI
KAIMU AFISA USHIRIKA MKOA WA NJOMBE BWANA EXAUD SAPALI AKITOA USHAURI JUU YA KUIFUTA BODI YA CHAMA
MUWAKILISHI TOKA BANK YA CRDB YA NJOMBE MJINI
MENEJA WA SACCOS YA NJOMBE MJINI PATRYOBA KYANDO AKITOA TAARIFA YA HESABU ZA MAPATO NA MATUMIZI YA SACCOS HIYO
WAJUMBE NA WANACHAMA WA SACCOS YA NJOMBE MJINI WAKISIKILIZA NA KUCHANGIA HOJA JUU YA CHANGAMOTO MBALIMBALI ZINAZOIKALI SACCOS PAMOJA NA KUSHAURI NAMNA YA KUIENDESHA ILI WANACHAMA WANUFAIKE NAYO
AFISA USHIRIKA WA HALMASHAURI YA MJI WA NJOMBE BWANA HERRISON NYAMBO AKITOA TAARIFA YA UKAGUZI WA SACCOS HIYO
Wanachama wa Chama cha Ushirika cha Akiba na Mikopo cha Wafanyabiashara SACCOS Mjini Njombe Wameuagiza Uongozi wa Bodi Hiyo Kufuatilia Marejesho ya Madeni Yote Kutoka Kwa Wanachana wa Saccos Hiyo Ambao Hawajaresha.
Aidha Wanachama Hao Pia Wameazimia Kuivunja Bodi Hiyo Ifikapo Mwakani endapo haitakamilisha kufuatilia madeni yaliokopeshwa na kwamba hali hiyo itakuja Kutokana na Utendaji Mbovu wa Bodi Hiyo Pamoja na Kutokuwa na Ushirikiano wa Utendaji Baina ya Uongozi wa Bodi na Wanachama.
Wakiongea Kwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka Wanachama wa SACCOS Hiyo Wameomba Kurekebishwa Kwa Mapungufu Yaliyopo Ikiwemo Kutowafikia Wanachama , Kutofuatilia Kikamilifu Madeni Kwa Wanachama Wake.
Ernest Nyandoa ni Mwenyekiti wa SACCOS Hiyo Ambaye Amekiri Kuwepo Kwa Mapungufu Yaliyojitokeza na Kuahidi Kuyafanyia Kazi Huku Akiwataka Wanachama wa Chama Hicho Kutoa Taarifa Pale Wanapoona Kuna Tatizo Kwa Uongozi wa Bodi na Watumishi wa SACCOS Hiyo .
Akizungumza Kwenye Mkutano Huo Kwaniaba ya Mgeni Rasmi , Afisa Ushirika wa Halmashauri ya Mji wa Njombe William Kinyaga Amewataka Wanachama na Viongozi wa Bodi Hiyo Kuondoa Tofauti Zao Ili Kuweza Kukijenga Chama Chao.
Katika Mkutano Huo Wanachama wa Saccos Hiyo Wamepatiwa Elimu Kutoka Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa NSSF Huku Afisa Mwandamizi wa NSSF Mkoa wa Njombe Ngusa Somolo Amewashauri Wananchi Kujiunga na Vyama Vya Ushirika Ili Wapate Mikopo Kutoka Kwenye Mfuko Huo .
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment